ZIARA YA PINDA MKOANI SHINYANGA

Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafunzo ya ukatibu muhtasi wakati alipozindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo Februari 26, 2012 .(Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mbunge wa Solwa Ahmed Ali Salum (mwenye kaunda suti) akisakata zeze katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda kwenye eneo la hospitali ya Iselamagazi, Shinyanga Februari 26, 2012 (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Msanii wa ngoma ya asili ya Kisukuma (jina halikupatikana) akionyesha fiisi wakati kikundi chake kilipotumbuiza katika mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katika kijiji cha Chela wilayani Kahama Februari 25, 2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
skari wa Jadi yaani Sungunsu wa jimbo la Solwa wakicheza ngoma yao wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokagua ujenzi wa hospitali ya Iselamagazi na na kuhutubia mkutano wa hadhara akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 26,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Mpiga zeze wa Kijiji cha Iselamagazi katika jimbo la Solwa Shinyanga (jina halikupatikana) akitumbuiza wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipokagua ujenzi wa hospitali na kuwahutubia wananchi wa kijiji hicho akiwa katika ziara ya mkoa wa Shinyanga Februari 26, 2010. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akizindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 26, 2012. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Shinyanga, Ally Nasoro Rufunga. (Picha na Of Ofisi ya Waziri Mkuu)
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akikagua mafunzo ya ushonaji wakati alipozindua Chuo cha VETA cha Shinyanga akiwa katika ziara ya mkoa huo, Februari 26,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
Wasanii wa ngoma ya Kisukuma ya Buyeyewakicheza ngoma hiyo wakati Waziri Mkuu, Mizengo Pinda alipohutubia mkutano wa hadhara kwenye uwanja wa Shycom Mjini Shinyanga, Februari 26,2012. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI