UPUNGUZAJI UMASIKINI UENDANE NA KUKABILIANA NA MABADILIKO YA TABIA NCHI

Mkurugenzi Mtendaji wa TASAF Ladislaus Mwamanga akitoa hotuba kwenye katika Warsha ya wadau wanaohusika na masuala ya kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi sambamba na kuondoa umasikini. warsha hiyo Imeandaliwa na Benki ya Dunia na kushirikiana na TASAF kufanyika jijini Machi 20.2012. Picha zote na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO
Mkufunzi kutoka Red-Cross Pablo Suarez akitoa mafunzo kwa vitendo kwa wanawarha hao leo.
Wadau mbalimbali wakiwa na wakufunzi wakishirikana katia mazoezi kwa vitendo ili kuchangamsha mwili katika warsha hiyo.
NA MAGRETH - KINABO
MKURUGENZI Mtendaji wa Mfuko wa Hifadhi ( TASAF),Ladislaus Mwamanga ametoa changamoto kuwa huondoaji wa umasikini katika jamii huendane sambamba na jinsi ya kuweza kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, ikiwemo athari za maafa.
Kauli hiyo ilitolewa leo wakati akifungua mkutano wa jinsi ya kuoanisha namna ya kuondoa na umasikini na kukabiliana na mabadiliko ya tabia na maafa uliofanyika kwenye hoteli ya Serena jijini Dares Salaam ambao umehusisha wadau kutoka serikalini, asasi za kiraia, mashirika yasiyoya kiserikali na taasisi zinazohusiana na utafiti.
“Kumekuwapo na matukio ya kuongezeka kwa joto na mabadiliko ya tabia nchi hali inayoathiri uchumi na maisha ya jamii. Mabadiliko ya tabia nchi , madhara yanayotokana na maafa, ikiwemo umasikini ni changamoto zinazotukabili hivi sasa.
“Ni lazima upunguzaji wa umasikini uendane sambamba na kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, huwezi ukazuia tatizo moja ukaliacha lingine,” alisema Mwamanga.
Aliongeza kuwa tafiti mbalimbali zimeonyesha kuwa uwezeshaji wa wananchi kiuchumi kupitia miradi mbalimbali hautaweza kufanikisha malengo ya maendeleo ya milinea ikiwa masuala yote hayatakwenda pamoja.
Mwamanga alisema lengo la mkutano huo ni kujenga uelewa kwa wadau mbalimbali jinsi ya kubuni mbinu za kuikinga jamii ili iweze kuondokana na matatizo hayo.
Aliongeza baada ya mkutano huo, wadau hao watatoa mafunzo katika jamii ya watu masikini kwa kutumia uhawilishaji fedha katika,(kuwapatia kipato), ambao wenye uwezo wa kufanya kazi , kuwapatia ajira na kuhamasisha jamii iweze kupata kipato kwa kutumia miradi mbalimbali na kuweka akiba kwa ajili kuongeza mingine.
Alisema TASAF iko tayari kuendelea kufanya kazi na wadau na nchi mbalimbali ambapo itaingiza katika utekelezaji wa mkakati wa awamu ya tatu wa mwaka 2012 - 2022 wa ikiwa ni hatua ya kukabiliana na changamoto hizo.
Aidha Mwamanga alisema TASAF kwa kushirikiana na Benki ya Dunia(WB) ambao ndio waandaji wa mkutano huo wameshaanza kutekeleza masuala hayo kwa kuingiza kwenye utekelezaji wa mipango yao ili kuweza kupunguza tatizo ya umasikini sugu unaochangia mabadiliko ya tabia nchi, mafuriko na ukame.
Naye Mwakilishi wa WB, ambaye Mwandamizi wa yanayohusiana na Jamii ,Ida Manjolo alisema uhamasishaji wa elimu hiyo itatolewa katika ngazi mbali za kijiji , wilaya na mikoa kwa wananchi kuhusu maendeleo yao kupitia wadau hao .

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI