Arusha Aprili 30, 2012 (EANA) – Nchi
wanachama wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) zinatakiwa kuunganisha nguvu zake
kwa pamoja ili kuzuia na kupambana na fedha haramu na ongezeko la ufadhili wa
vitendo vya kigaidi katika kanda hiyo.
‘’Nchi za EAC zinaweza kufanikiwa katika
kuzuia na kupambana na fedha haramu na ufadhili wa ugaidi kupitia juhudi za
pamoja,’’ alisema Waziri wa Usalama wa Burundi, Gabriel Nizigama wakati wa
kufungua warsha ya siku nne ya wataalam juu ya fedha haramu na ufadhili wa
ugaidi, mjini Bujumbura, Burundi, Juzi.
Kanda hiyo, alisema, inahitaji hatua
maalum ya kutambua na kuzuia shughuli za kihalifu kupitia uhifadhi wa kumbukumbu
na utambuzi wa wateja na pia utoaji taarifa haraka juu ya shughuli au watu
wanaotiliwa mashaka.
Warsha hiyo inayodhuriwa na wataalamu wa
kupambana na fedha haramu,kitengo cha usalama wa fedha, mamlaka za mapato,
wanasheria, polisi na maafisa usalama imeandaliwa na EAC kwa kushirikiana na
serikali ya Australia.
Warsha hiyo ni matokeo ya uamuzi wa
mkutano wa nne wa Baraza la Kisekta ya Usalama ambao ulitambua kwamba fedha
haramu ni tishio kwa mtangamano wa EAC.
Naye Naibu Katibu Mkuu wa EAC,
anayeshughulikia Shirikisho la Kisiasa, Beatrice Kiraso, alisema kwamba kadiri
mtangamano wa EAC unavyozidi kuimarika, ni dhahiri kwamba kuwepo kwa vitendo vya
uhalifu hakukwepeki.
‘’Tuna wajibu wa kulinda miundombinu yetu
ya fedha na utulivu wa uchumi wetu kama manufaa ya mtangamano wetu yanatakiwa
yaonekana,’’ alisisitiza na kuongeza kwamba uhalifu kama usafirishaji wa fedha
haramu na ufadhili wa vitendo vya kigaidi lazima vipigwe vita
vikali.
Alisema vinginevyo uhalifu huo utaharibu
maendeleo ya kiuchumi ndani ya kanda, kuwatisha wawekezaji na kuharibu usalama
na utulivu uliopo ndani ya nchi za EAC, alieleza Kiraso katika hotuba iliyosomwa
kwa niaba yake na Mtaalamu wa EAC wa Masuala Amani na Usalama, Leonard
Onyonyi.
Mwakilishi wa serikali ya Australia, Mike
Petty kwa upande wake alisema ushirikiano wa kikanda na kimataifa ni muhimu
katika mapambano dhidi ya uhalifu kwa sababu utandawazi siyo tu kwamba unaleta
teknolojia na jamii pamoja bali pia wahalifu na uhalifu hatari.
NI
Comments