MAZOEZI YA PAMOJA MISS UKONGA, MISS TABATA


Miss Ukonga 2012 walio chuchumaa wakiwa katika picha ya Pamoja na wartembo wa Miss Tabata 2012 wakati walipofanya mazoezi ya pamoja jana.
WAREMBO wa vitongoji viwili vya Ukonga na Tabata jana walifanya mazoezi ya pamoja katika kuleta ushirikiano na kujenga urafiki baina ya warembo hao katika fani ya urembo.

Warembo wa Tabata waliwatembelea wenzao wa Ukonga katika kambi yao ya mazoezi iliyopo Ukonga Hill Tech Bar maeneo ya Minazi Mirefu au maarufu Banana.

Vitongoji vya Ukonga na Tabata warembo wake watakao shinda wanataraji kukutana katika Kambi ya kanda ya Ilala kabla ya kwenda kushiriki shindano la taifa la Miss Tanzania 2012.

Wakizungumza jana baadhi ya warembo wa Ukonga wamesema ushirikiano wao huo na wenzao wa Tabata unawapa uwezo wa kijiamini na kupata nafasi ya kujifunza kile ambacho wenzao wanakifanya au wamejifunza ikiwa ni pamoja na utembeaji, uongeaji wa kati wa kujitambulisha na vitu vingine vingi.

“Tunawashukuiru sana waandaji wetu, maana mbali ya kuwa tunapata wageni wa aina mbalimbali ambao ni wadau wa urembo lakini leo tupo na washiriki wenzetu wa tabata ambao tunaimani tutakutana katika shindano la Ilala”, alisema Amina Sangawe.

Nae Suzanne Deodatus ambaye ni Mshiriki kutoka Tabata alisema wamepata fursa ya kujifunza mambo kabdhaa na wamefurahi sana kuwatembelea warembo wa Ukonga na kufnya nao mazoezi ya pamoja.

Mapema Mwezi huu warembo wa Ukonga waliwasindikiza Miss Tabata 2012 katika show yao kubwa ya Utambulisho iliyofanyika katika Ukumbi wa Dar West Tabata.

Shindano la Miss Ukonga 2012 linataraji kufanyika Mei 5, mwaka huu na lile la Tabata linataraji kufanyika mapema mwezi Juni.
Miss Ukonga 2012 wakicheza mziki wa ufunguzi
Baadhi ya waremnbo wa Tabata wakipita kwa mwendo wa madaha.
Warembo Ukonga wakicheza ngoma.
Warembo wa Miss Ukonga 2012 wakimwangalia Mshiriki mwenzao kutoka Tabata akipita mbele yao.
Ngoma ya asili nayo imo na hapa ni kucheza kwenda mbele.
Mwandaaji wa Miss Tabata, Freddy Ogot (katikati) akiwaeleza jambo waandaaji wa Miss Ukonga 2012.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AKARIBISHWA KIMILA NYUMBANI RUVUMA