MTOTO WA AJABU AZALIWA SONGEA

KATIKA hali isiyokuwa ya kawaida, mtoto wa ajabu amezaliwa katika Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma, mjini Songea, ambapo maumbile yake ya sehemu za siri yako kichwani.

Tanzania Daima limeshuhudia tukio hilo la mtoto huyo ambaye amehifadhiwa katika chumba cha uangalizi maalumu katika hospitali hiyo, kwa lengo la kujaribu kupunguza msongamano wa watu ambao wamekuwa wakimiminika kumshuhudia.

Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali hiyo, Mathayo Chanangula, alisema mtoto huyo alizaliwa Aprili 25, mwaka huu, saa saba mchana akiwa na uzito wa kilo 1.9 licha ya kutimiza miezi tisa ya kuzaliwa.

Chanangula lifafanua kuwa kwa kawaida mtoto anatakiwa kuzaliwa na uzito wa kilo 2.5. Pia alieleza sababu za kitaalamu zilizosababisha mtoto huyo kuzaliwa katika hali hiyo kuwa ni unywaji wa dawa zisizostahili kwa mama mjamzito kabla ya kutimiza miezi mitatu ya ujauzito.

Mtoto huyo kila anaponyonya, sehemu hiyo za siri ya jinsia ya kiume iliyo kichwani kwake inasimama kama vile anataka kujisaidia haja ndogo.

Naye muuguzi mkunga wa hospitali hiyo, Philomena Mwingira, alisema mtoto huyo amezaliwa akiwa na maumbile yasiyo ya kawaida, hivyo hawawezi kumuacha nje badala yake wameamua kumhifadhi katika chumba maalumu na kwamba wanaendelea kumfariji mama huyo kukubaliana na hali hiyo.

Wazazi wa mtoto huyo, Stumai Ausi na Abdallah Saidi, wakazi wa Msamala mjini Songea, wameiomba jamii na wataalamu mbalimbali kuwasaidia kumaliza tatizo la mtoto wao ili aweze kurejea katika maumbile yake ya kawaida.


juu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

MONGELLA AKABIDHIWA ‘MIKOBA’ RASMI YA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA*

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI