KAIMU KAMANDA KIHENYA KIHENYA AKIWAONESHA WAANDISHI WA HABARI SIRAHA MBILI ZA KIVITA AINA YA SMG ZILIYO KAMATWA
Na Pardon Mbwate na Felister Elias wa Jeshi la Polisi -Kigoma
Jeshi
la Polisi mkoa wa Kigoma linawashikilia watu wanne wakiwemo wawili raia
wa nchi jirani ya Burundi kwa tuhuma za kupatikana na silaha mbili za
kijeshi aina ya SMG na risasi mbili.
Kaimu
Kamanda wa Polisi mkoani Kigoma SSP Kihenya wa Kihenya, amewataja Raia
hao wa Burundi waliokamatwa kuwa ni Ndolimana Alfred Ndoli(29), mkaazi
wa Lutana Kiharu na Bosco Yohana Gabriel(35), mkaazi wa Kibimba Giharu
ambao walikamatwa katika kijiji cha Nguruka silaha moja wakiwa na SMG
moja yenye namba 56–2500509
Kamanda
Kihenya amewataja Watanzania waliokamatwa sambamba na Warundi hao kuwa
ni Matata Chubwa Ntasamba(36), mkaazi wa kijiji cha Kitanga Wilaya ya
Kasulu na Ndegeya Medard(28), mkazi wa kijiji cha Kitanga wilaya ya
Kasuliu mkoani Kigoma walikamatwa katika Kitongoji cha Lugongoni tarafa
ya Nguruka wakiwa na magazini mbili za SMG na moja kati ya hizo ikiwa na
risasi mbili.
Amesema
kuwa silaha iyoyo na risasi ilipatikana katika kandokando ya mto
Ruguzye uliopo katika pori la kijiji cha mabama wilayani Kinondo baada
ya kutelekezwa na majambazi wasiojulikana kufuatia msako mkali
unaoendelea mkoani humo wa kutafuta silaha na majambazi wa kutumia
silaha.
Katika
tukio lingine Kamanda Kihenye amesema mkazi mmoja wa Kitongoji cha
Mrusi mjini Kasulu, Elizabeth Kanyungu(46), alikutwa akiwa amejinyonga
kwa kutumia kamba ya katani ndani ya nyumba yake.

Comments