Hii ni Kampeni ndani ya Vitongoji vyote 374 vya Jimbo la Musoma Vijijini kuwafuata wapiga kura majumbani, kwenye vituo vya usafiri, senta za biashara, mialoni, vijiwe vya bodaboda,magenge ya mama lishe, n.k.

Lengo la kuwafuata huko waliko ni kuendelea kueleza utekelezaji
wa miradi ya maendeleo ya kila kijiji na vitongoji vyake kwa miaka mitano iliyopita na ile mitano ijayo (Ilani za Uchaguzi za CCM za 2020-2025 & 2025-2030), na Dira ya Maendeleo ya Taifa (2025 -2050)

Vilevile, Timu yetu ya Kampeni ikiwajumuisha Viongozi kwenye Vitongoji hivyo 374, itahamasisha WAPIGA KURA wajitokeze kwa wingi kwenda kupiga kura (tarehe 29 Okt 2025) na kuwachagua wagombea wote wa CCM wakiongozwa na Mgombea Urais Dkt Samia Suluhu Hassan, Mgombea Ubunge wa Jimbo letu na Wagombea Udiwani 21 wa kata zetu zote. 

Kazi na Utu,
Tunasonga Mbele.

Timu ya Kampeni
CCM - Jimbo la Musoma Vijijini.
Jumapili Okt 19, 2025.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

KIGOGO WA CHADEMA AHAMIA CCM

RAIS SAMIA SIO RAIS JOYCE BANDA WA MALAWI, TANZANIA SIO KENYA

DKT. SAMIA AAHIDI KUJENGA CHUO CHA UHASIBU SONGEA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA