MBATIA AONGOZA KIKAO CHA HALMASHAURI KUU YA CHAMA CHA NCCR-MAGEUZI

Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha NCCR-Mageuzi James Mbatia, akiongoza kikao cha Halmashauri Kuu ya Chama hicho leo kilichofanyika Hoteli ya Mbezi Garden Dar es Salaam.

Katibu Mkuu wa Chama hicho, Samuel Ruhuza akiwa kwenye kikao hicho.
(PICHA HABARI NADOTTO MWAIBALE)


Naibu Katibu Mkuu wa Chama hicho Tanzania Visiwani, Mussa Kombo akiwa katika kikao hicho

Mweka Hazina Mkuu wa Chama hicho, Mariam Mwakingwe akiwa kwenye kikao hicho
Muasisi ambaye pia ni mwanachama mwenye kadi namba tatu ya Chama hicho, Emanuel Sirikwa(kushoto), akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Mkutano huo kutoka mkoani Kagera, Peterson Mshenyelwa wakati wa kikao hicho.
Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho

Baadhi ya wajumbe wakiwa kwenye kikao hicho



Serikali yatakiwa kuondoa kesi dhidi ya madaktari

Na Dotto Mwaibale

SERIKALI imetakiwa kuifuta kesi iliyofungua Mahakama Kuu ya Tanzania kupinga mgomo wa madaktari na kurudi katika meza ya mazungumzo na wanataaluma hao ili kuyanusuru maisha ya watanzania.

Rai hiyo imetolewa na Mwenyekiti wa Chama cha NCCR-Mageuzi, James Mbatia wakati akifungua mkutano Mkuu wa Halmashauri ya chama hicho Dar es Salaam leo.

Alisema ni muda muafaka kwa serikali kwenda mahakani kufuta kesi hiyo na kurejea kwa mara nyingine katika meza ya mazungumzo na madaktari hao badala ya kukaa kimya huku watanzania wakendelea kukosa huduma za matibabu na wengine wakipoteza maisha.

" Serikali ilikimbilia mahakamani kuzuia jambo hilo lisizungumziwe lakini kipi bora kati ya uhai wa binadamu kupoteana na suala hilo kuendelea kuwa mahakamani huku watanzania wakiendelea kufa" alihoji Mbatia.

Alisema Serikali inatakiwa isiweke kiburi kwa jambo hilo na madaktari nao walegezeze uzi wao na kukaa na serikali katika meza ya majadiliano.

Alisema hali hii ni changamoto kwa serikali kwani itapitiwa na watanzania na kuwa itabaki katika kumbukumbu zao hivyo ni wajibu kwa serikali kulimaliza jambo hilo.

Alisema wakati serikali ikidai haiwezi kuzungumzia masuala ambayo yapo mahakamani hasa hilo la mgomo wa madaktari juzi bungeni limeongolewa sakata la fedha za Deci baada ya mbunge wa Kawe, Halima Mdee kuibana serikali na kutaka kufahamu imeokoa kiasi gani cha fedha katika mchezo wa upatu uliokuwa ukiendeshwa na taasisi ya Deci.

"Unaona jinsi serikali inavyojichanganya wakati inadai inasimamia utawala wa sheria kwa kuto ingilia mahakama katika masuala makubwa na muhimu kwa taifa hawataki kuzungumzia kwa kivuli cha mahakama lakini haya yasiyohusu uhai wa binadamu wanayapa kipaumbele si ni hatari hii" aliongeza Mbatia.

Akizungumzia misamaha ya kodi amesema ni eneo ambalo linadidima mno maisha ya mtanzania kwani katika kipindi cha miaka mitano ilisamehe kodi ya trioni 5 jambo ambalo linaturudisha nyuma kimaendeleo.

Akitolea mfano taasisi ya Agakhan Foundation alisema tangu wa Serikali ya awamu ya kwanza ilitiliana mkataba wa kusamehewa kulipa kodi kwa vile inatoa huduma kwa jamii.

Alisema taasisi hiyo licha ya kusamehewa kulipa kodi lakini wananchi hawanufaiki nayo kutokana na huduma za matibabu wazitoazo kuwa ni kubwa ukilinganisha na Hospitali zingine kubwa ambazo zinatoa huduma za matibabu.

Alisema baadhi ya makampuni ya ujenzi yamekuwa yakipunguziwa gharama za ununuzi wa saruji kwa mgongo wa taasisi hiyo ambapo nao uenda kuiuza kwa bei ya soko lililopo hali ambayo ni ya kulididima taifa.

Alisema msamaha huo wa kodi upo hadi katika Shule mbalimbali za taasisi hiyo ambazo huduma wazitoazo kwa jamii zinaweza zisiwe sahihi kwa kumsaidia mwananchi na hali hiyo ni mwanya mwingine wa kuwaibia watanzania hivyo kuwa ni pango la kifisadi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI