MISS UNIVERSE NI WINIFRIDA DOMINIC.




Miss Universe 2012, Winfrida Dominic, baada ya kutangazwa kushikilia taji hilo


Mwandaaji wa Miss Universe, Mariam Sarungi (kushoto), akimpongeza Winfrida Dominic.
Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora
Mshindi wa Shindano la Miss Universe 2012 (katikati) akiwa kwenye picha ya pamoja na mshindi wapili Bahati Chando (kushot) na mshindi watatu Dorice Mollel, mara baada ya kukabidhiwa taji hilo kwenye fainali za shindano hilo zilizofanyika jana jijini Dar es Salaam
Mrembo aliyekuwa akishikilia taji hilo la Miss Universe Nelly Kamwelu (kushoto) akikabidhi taji hilo kwa mshindi mpya Winifrida Dominic jana Usiku.
Baadhi ya mashabiki wa shindano hilo walihudhuria kushuhudia mshindi anavyopatikana.

Warembo wakiwa kwenye muonekano tofauti wakati wakipita mbele ya Mashabiki wa shindano hilo.

Warembo waliofanikiwa kuingia tano bora


Majaji wakichakarika kusaka mshindi wa shindano hilo



Winfrida atwaa taji la Miss Universe 2012

Na Dotto Mwaibale
MREMBO Winfrida Dominic (19) wa Dar es Salaam ameshinda taji la Miss Universe Tanzania, baada ya kuwashinda washiriki 16 katika fainali za mashindano hayo zilizofanyika kwenye Ukumbi wa Makumbusho ya Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na ushindi huo, Winfrida alipata ushindani mkali hasa katika hatua ya tano bora, ambapo warembo walijibu maswali mbalimbali kabla ya kutangazwa mshindi.

Winfrida, alionekana kujiamini tangu mwanzo wa mashindano hayo, na hiyo kuwa silaha kubwa katika mafanikio yake. Uzuri wake wa asili pia ulichangia kupata ushindi na kupata tiketi ya kuiwakilishaTanzania katika mashindano ya dunia yaliyopangwa kufanyika Desemba katika nchi itakayotangazwa baadaye.

Mbali na kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya kimataifa ya Miss Universe, mrembo huyo pia alizawadiwa sh. milioni 3, na kupewa ofa ya kwenda kusoma nchini Marekani katika Chuo cha New York Film Academy.

"Ndoto yangu imetimia, nilipoamua kushiriki katika mashindano haya, lengo langu lilikuwa ushindi, ushindani ulikuwa mkubwa sana na hasa hatua ya tano bora, namshukuru Mungu kwa kuniwezesha kushinda taji hili," alisema Winfrida.

Nafasi ya pili katika mashindano hayo ilikwenda kwa Bahati Chando (20), pia wa Dar es Salaam, ambaye alipata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Earth na kuzawadiwa kitita cha sh milioni 1, huku Dorice Mollel (21) akiibuka katika nafasi ya tatu na kupata nafasi ya kuiwakilisha Tanzania katika mashindano ya Miss Tourism Queen International na kitita cha sh 500,000.

Dar es Salaam ilitawala mashindano hayo, kwani hata nafasi ya nne na tano zilichukuliwa na Kundi Mligwa (23) na Lilian Kolimba, ambao walizawadiwa sh 100,000 kila mmoja


Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI