RAIS KIKWETE AKUTANA NA WATENDAJI WAKUU WA MAKAMPUNI MBALIMBALI YA KIMAREKANI WANAOTEMBELEA TANZANIA

Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na wanafunzi wa Kimarekani na waalimu wao pamoja na Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe John Haule, Balozi wa Marekani nchini, Mhe na Balozi wa Tanzania nchini Marekani Mhe Mwanaidi Sinare Maajar. Wanafunzi hao  wanachukua masomo ya lugha ya Kiswahili katika Chuo Kikuu cha Zanzibar ( SUZA). Walikuwa  wameongozana na  Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Rais Kikwete  Ikulu jijini Dar es salaam leo  Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani
Rais Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na Watendaji Wakuu wa Makampuni mbalimbali kutoka Marekani walipomtembelea Ikulu jijini Dar es salaam leo Juni 30, 2012 katika ziara yao ya siku kadhaa ya kuvumbua tanzania (Discover Tanzania VIP CEOs tour) iliyoandaliwa na ubalozi wa Tanzania Marekani. Hii ni mara ya pili kufanyika ziara kama hii, ambapo pamoja na kuwakaribisha tena Rais Kikwete alisema amefurahishwa sana kwa wageni hao kuchagua kutembelea hifadhi za wanyama za kusini mwa nchi (Selous na Ruaha) vyenye wanyama wengi na vivutio ambavyo havipatikani kwingine kokote kama vile makundi ya mbwa mwitu  ambayo kwa muda mrefu sasa yametoweka mbuga za Kaskazini.

PICHA NA IKULU

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI