TAASISI YA MASHEIKH NA WANAZUONI WA KIISLAMU TANZANIA YAUNGA MKONO KAULI YA MUFTI, YASEMA HAIONI TATIZO LA SENSA YA WATU NA MAKAZI 2012


Sheikh Hamis Mattaka(kushoto) akitoa tamko mbele ya  waandishi wa habari kwa niaba ya Mwenyekiti wa jopo la Masheikh wanazuoni wa kiislam Tanzania  kuhusu mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba, Sensa ya watu na Makazi na Hali ya Zanzbar leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Sheikh Iddi Simba.
 
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Dar es Salaam.
Taasisi ya masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imeunga mkono kauli iliyotolewa hivi karibuni na Sheikh mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban  Simba ya kuwataka waislamu na watanzania  kote nchini kushiriki kikamilifu katika Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika  Agosti 26 mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mwenyekiti wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania Sheikh Hamis Mattaka amesema hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa baadhi ya makundi yanayowahamasisha waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kutoshirika zoezi la Sensa ya watu na makazi.
Amesema  wao kama jopo la wanazuoni hawaoni tatizo la zoezi hilo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na kuongeza kuwa  Sensa ya watu na makazi ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Jopo hilo  limeiomba serikali kuweka sheria itakayozuia utoaji wa takwimu zinazohusu dini za watanzania zinazotolewa na vyanzo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kuwa kipengele hicho si sehemu ya sensa nchini.
“Tunajua kuwa serikali ilikua na nia njema kukiondoa kipengele cha dini katika Sensa hapana budi nia njema hiyo ya serikali ilindwe kwa kuweka sheria itakayozuia kutoa takwimu zinazohusu dini za watanzania” amesema Sheikh Mattaka.
Amefafanua kuwa Sensa ya awali ya mwaka 1957 kipengele cha dini kilihusishwa na baadaye kuondolewa katika Sensa zilizofuata kwenye madodoso ya kukusanyia takwimu z

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI