WAZIRI MKUU ATAKA WAJASIRIAMALI WAWE MAKINI


 
Waziri Mkuu, Mizengo Pinda akifurahia moja kati ya viatu vilivyoonyeshwa kwenye banda la Mareshi Shoe Maker  katika kilele cha sherehe za kutoa ruzuku kwa wajasiliamali waliofanya vizuri  katika Progamu ya fanikiwa kibiashara zilizofanyika kwenye viwanja vya Mnazi mmoja jijini Dar es salaam Juni 30,2012.Kulia kwake ni Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Uwezeshaji na Uwekezaji, Dkt, Mary Nagu na kulia Mwenyekiti  wawa Taasisi  ya Sekta Binafsi Tanzania, Mama Ester Mkwizu. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu)
 
 
WAZIRI MKUU Mizengo Pinda amewataka wajasiriamali wa kati na wadogo nchini wawe waangalifu na makini katika biashara wanazopanga kuzifanya kama kweli wanataka kufanikiwa maishani na akawaonya wale waliopata mbegu mtaji kuchukua tahadhari zaidi.
 
Ametoa onyo hilo leo mchana (Jumamosi, Juni 30, 2012) wakati akizungumza na wajasiriamali kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani ambao walihudhuria sherehe za kutoa zawadi kwa washiriki wa Programu ya Fanikiwa Kibiashara (Business Development Gateway - BDG) kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja jijini Dar es Salaam.
 
Naomba niwatahadharishe kuwa ujasiriamali unataka umakini wa hali ya juu. Mmoja wa Wajasiriamali mashuhuri huko Marekani aliwahi kutoa tahadhari kwa kusema: "Business is like oil, it won't mix with anything but Business" akimaanisha kwamba biashara ni kama mafuta ya kulainisha mitambo (oil) ambayo hayachanganywi na kitu kingine chochote, isipokuwa oil yenyewe. Tunahitaji uangalifu na umakini katika kufanya biashara zetu bila kuchanganya na mambo mengine
 
Amesema mtu anapochukua mkopo kwa nia ya kuanzisha biashara kisha akaamua kuoa mke wa tatu au kununua gari kwa kutumia fedha hiyo ya mtaji ni lazima atakwama kwa sababu atakuwa amechakachua dhima nzima ya ile biashara yake.
 
Alisema katika mabanda ya maonesho aliyotembelea leo, ameona changamoto kuu tatu ambazo zinahitaji kuangaliwa haraka ili kuinua soko la bidhaa za wajasiriamali hao.
 
Alizitaja changamoto hizo kuwa ni ukosefu wa vifungashio bora, ukosefu wa alama za viwango kutoka shirika la viwango nchini (TBS) na ukosefu wa alama ya biashara (bar code) katika bidhaa zao. “Bidhaa zenu ni lazima ziwe na vifungashio vizuri vyenye mvuto ili mnunuzi ashawishike kununua.”
 
“Nawasihi mfuate masharti ya shirika la viwango nchini ili bidhaa zenu zikubalike,  waoneni wahusika ili mpate bar code kwenye bidhaa zenu. Bidhaa zenu zikiwa na bar code zitakubalika kokote ulimwenguni,” alisisitiza.
 
Waziri Mkuu pia alisema anatatizwa na changamoto moja kuu ambayo ni ya kuhakikisha mpango wa BDG unaendelezwa ili uwanufaishe watu wengi zaidi. “Mpango huu umefikia mwisho, na umedumu kwa miaka minne tu. Mwenyekiti wa TPSF itabidi tuangalie hata uwezekano wa kukopa ili jambo hili zuri lisiishie hapa,” alisema.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI