YANGA KUTAMBULISHA NYOTA WAKE LEO

MABINGWA wa Kombe la Kagame, Yanga leo watawatambulisha nyota wake wapya katika mchezo wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya Express ya Uganda utakaofanyika kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Mashabiki wa Yanga watamshuhudia kwa mara ya kwanza beki Kelvin Yondani akiichezea timu hiyo tangu walipomsajili kutoka kwa mahasimu wao Simba.

Mbali ya Yondani wachezaji wengine watakaotambuliswa leo ni pamoja na Said Banahuzi, Juma Abdul, Nizar Khalfan, Frank Domayo, Simon Msuva, Ladislaus Mbogo na Ally Mustafa ‘Barthez’.

Kocha msaidizi wa Yanga, Fred Minziro alisema kikosi chake kipo tayari kwa pambano hilo."Ushindani ulioonyeshwa na wachezaji wangu katika mazoezi unatia faraja na naamini kikosi changu kitafanya vizuri katika mchezo wa leo," alisema Minziro.

Viingilio katika mchezo huo wa leo ni Sh 20,000 kwa VIP A, Sh15,000 kwa VIP B wakati viti vya Kijani ni Sh 5,000 na viti vya blue mzunguko Sh3,000.

Katika hatua nyingine ujio wa kocha mpya wa Yanga umezidi kuwa kitendawili baada ya uongozi wa klabu hiyo kushindwa kutoa kauli sahihi ya ujio wa kocha huyo.

Awali kulikuwa na taarifa kuwa aliyewahi kuwa kocha wa Taifa Stars, Marcio Maximo ndiye atakuja kuinoa timu hiyo ya Yanga, lakini mpaka sasa kocha huyo hajawasili.

Lakini hivi karibuni Katibu Mkuu wa klabu hiyo, Celestine Mwesigwa alikanusha ujio wa Maximo na kusema kuwa kuna makocha 25 ambao waliomba kazi ya kuinoa timu hiyo, ambapo wamewachuja na kubaki watatu.

Mwesigwa alisema kuwa bado wanaendelea na mchakato ili waweze kumpata kocha mmoja ambaye wanatarajia kumtangaza baada ya mchakato huo kumalizika.

Jana Afisa Habari wa Yanga, Louis Sendeu alisema kuwa mchakato huo bado unaendelea na siku yoyote wanaweza kumtangaza kocha huyo mpya wa klabu hiyo.

Wakati huohuo, Sendeu alikanusha ushiriki wa timu yao katika mashindano ya Kombe za Urafiki yanayotarajiwa kuanza Jumapili mjini Zanzibar.Cahnzo. gazeti la Mwananchi.

Alisema kuwa awali Chama cha Soka cha Zanzibar ( ZFA) kiliwapa taarifa, lakini walijua mazungumzo yataendelea ingawa haikuwa hivyo kwani walikuwa kimya na wanashangaa kuona wamepangwa kwenye ratiba ya mashindano hayo.

Alisema kuwa wao kama Yanga hawako tayari kushiriki mashindano hayo kutokana na ratiba yao kuwa ngumu na wanataka kutetea ubingwa wao wa kombe la mashindano ya Kagame.

''Hatutaweza kushiriki mashindano hayo kwa kuwa tunahofia wachezaji wetu kuumia kwa sababu viwanja vya Zanzibar siyo vizuri, pia sisi ndio mabigwa watetezi wa Kombe la Kagame hivyo tunataka kutetea kombe letu la Kagame,''alisema Sendeu.

Alisema wangekuwa tayari kushiriki mashindano hayo baada ya Kagame kwa sababu hawawezi kushiriki mashindano ya Kagame wakiwa na majeruhi wengi

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI