CODE HIZI ZIKO POA: Dimpoz kuzindua Video ya BADAYE Maisha Clab Jumapili hii


AU INGIZA HII 

MSANII wa Mziki wa Kizazi kipya anaetamba na nyimbo zake mbili za  Nai Nai na Badaye, na mshindi wa Tuzo mbili za Kili Music Award 2012, Omy Dimpoz anataraji kuzindua Video yake mpya ya Baadaye  katika ukumbi wa Club Maisha Septemba 9,2012 jijini Dar es Salaam.
 
Akizungumza na Blog hii, Meneja wa Msanii huyo, Mbaruku Issa ‘Mubenga’ alisema kuwa maandalizi yote yamekamilika na show itakuwa ya uhakika naya kuvutia.
 
Mubenga amesema Omy Dimpozy ameifanyia shooting video yake hiyo nchini Afrika Kusini.
Aidha Mubenga amesema kuwa kazi ya utayarishaji wa vuideo hiyo ulifwanywa na Adam Juma wa Visual Lab ambaye ndiye walisafiri nae hadi Afriia Kusini na wameshoot kwenye maeneo mazuri na ya kifahari yaliyopo nchini humo ambapo ameona utofauti mkubwa katika kufanya video nje na nyumbani.
 
“Kazi hii ni ya uhakika ambayo tunaizidua Jumapili hii na Video hiyo imefanyika Johannesburg mitaa ya Sendton na nikatika location kali na za uhakika,”alisema Mubenga. 

Amesema wasanii kadhaa watasindikiza uzinduzi huo akiwepo Chegge Chigunda, Suma Mnazareth na Nas 3 siku hiyo katika uzinduzi wa  video hiyo mpya na Dimpoz nae atakuwa katika muonekano tofauti si Dimpoz waliye mzoea.

Pia Meneja huyo wa Omy Dimpoz amesema akiwa nchini Afrika kusini Dimpoz alimshirikisha Model ambaye amekuwa akifanya kazi na wasanii wengi wakali wa Mziki nchini humo anaejulikana kwa jina la Tully Tshabalala. 
 
“Wimbo ni mkali na mashabiki wanaukubali vilivyo na tunaomba mashabiki wa Bongo Fleva wakae tayari kwa video hiyo mpya itakayoanza sasa kuchezwa katika vituo vya Televisheni nchini na kumbi za burudani baada ya uzinduzi huo,” alisema Mubenga.
 
Mubenga amewakata wakazi wa jiji la Dar es Salaam ambao ni mashabiki na wapenzi wa muziki wa kizazi kipya kujitokeza kwa wingi kumpa support Dimpoz katika uzinduzi huo wa aina yake katika Club Maisha Oyster bay jijini la Dar es Salaam jumapili.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

WAZIRI BASHE APIGA MARUFUKU WASIOSOMEA KILIMO KUUZA PEMBEJEO

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA

DK. KIKWETE AZINDUA KITUO CHA AFYA KIZIMKAZI, APONGEZA MAENDELEO ZANZIBAR

KOCHA WA MAMELODI ASIMAMISHWA KWA KUWAPIGA CHABO WACHEZAJI WAKE WA KIKE