NIZAR AING'ARISHA YANGA AKITOKEA BENCHI, SALAMU ZAO SIMBA ZENJI

Shujaa wa leo Nizar

Na Prince Akbar
YANGA imeibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya African Lyon katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, uliomalizika hivi punde kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Shukrani kwake kiungo anayecheza kwa nadra kwenye timu hiyo, Nizar Khalfan aliyefunga mabao ya ushindi dakika ya 65 na 88, akitokea benchi kuchukua nafasi ya Frank Domayo.
Nizar alifunga bao la pili, sekunde chache baada ya Benedictor Mwamlangala kuisawazishia African Lyon bao lililodumu tangu dakika ya 17, baada ya Nahodha wa Yanga, kutangulia kufunga dakika ya 17.
Ushindi huo, unaifanya Yanga ifikishe pointi saba, baada ya kucheza mechi nne na kupanda hadi nafasi ya nne kwenye msimamo wa ligi, ikiwa inalingana na Coastal kwa pointi na wastani wa mabao, ingawa Coastal wako nyuma kwa mechi moja.
Simba bado inaongoza ligi hiyo, kwa pointi zake 12, ikifuatiwa na Azam yenye pointi 10.  
Yanga SC; Ally Mustapha 'Barthez', Mbuyu Twite, Oscar Joshua, Kevin Yondan, Nadir Haroub 'Cannavaro', Athumani Iddi 'Chuji',  Simon Msuva, Frank Domayo/Nizar Khalfan, Didier Kavumbagu, Hamisi Kiiza/Said Bahanuzi na Haruna Niyonzima. Kwa Hisani ya Bin Zubeiry Blog.











Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI