ASAS ATOA MSAADA WA MIFUKO 200 YA SARUJI KILOLO

Mfanyabiashara  maarufu  mkoani Iringa na Kada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Salim Abri Asas ( wa pili  kulia) akikabidhi msaada wa  mifuko 200 ya saruji yenye thamani ya zaidi ya sh. mil. 3 .2 kwa Mkuu wa Wilaya ya Kilolo, Gerald Guninita jana ofisini kwake  mjini Iringa. Wanaoshuhudia ni Mwenyekiti  wa Halmashauri ya Kilolo, Joseph Mhumba  na Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya hiyo, Momahend Gwalima (PICHA NA FRANCIS GODWIN)

Na Francis Godwin,Iringa

MFANYABIASHARA mkoani Iringa na kada wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa  wa Iringa  Salim Abri Asas ametoa msaada wa mifuko 200 ya Saruji yenye thamani ya  zaidi ya shilingi milioni 3.2  kwa ajili ya  kusaidia  ujenzi  wa mabweni ya wasichana katika  shule  nne za sekondari  wilaya ya Kilolo mkoani Iringa.

Akikabidhi  msaada  huo jana  ofisini kwake  Asas alisema  kuwa amelazimika  kuchangia  ujenzi huo wa mabweni ikiwa ni  sehemu ya  kuiunga mkono serikali  iliyopo madarakani  chini ya Rais Jakaya  Kikwete ambapo suala la elimu  limekuwa  likipewa kipaumbele  zaidi.

Alisema  kuwa mbali ya  kuchangia ujenzi huo katika  wilaya ya  Kilolo pia amepata kufanya hivyo katika   Halmashauri ya  Manispaa ya Iringa na maeneo mengine  ya mkoa  wa Iringa.

Alisema  kuwa wilaya hiyo ya  Kilolo kupitia mkuu  wa wilaya  Gerald Guninita waliandika barua kwake  kuomba kusaidiwa ujenzi wa  shule za sekondari na mabweni katika  wilaya  hiyo ya  Kilolo.

Kwa  upande  wake  mkuu  wa  wilaya ya  Kilolo Bw Guninita  mbali ya  kumpongeza Asas ambaye pia ni mmoja kati ya  wafanyabiashara  mkoani Iringa  bado  aliomba  wadau wengine wa  elimu  katika  mkoa  wa Iringa wakiwemo  wafanyabiashara  kujitokeza  kuchangia  maendeleo ya  elimu katika  wilaya hiyo ya Kilolo.

Hata  hivyo  mkuu  huyo  wa wilaya  alisema  kuwa saruji  hiyo   itagawanywa mifuko 50 kwa   shule  nne  za  sekondari ambazo zinaendelea na ujenzi  wa mabweni ya  watoto  wa  kike.

Alizitaja  shule za  sekondari ambazo zitanufaika na msaada  huo  kuwa ni  sekondari ya Uhambingeto,Gangwa ,Ukwega na Masisiwe .

Aidha  mkuu  huyo  wa  wilaya  ametangaza  kuwachukulia hatua kali  wale  wote  wanaowapa  mimba  wanafunzi na  kuwa tayari ameagiza  viongozi kuanza  kuwasaka wahusika  wa mimba za  wanafunzi ili  kukamatwa na kufikishwa mahakamani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE