MTITI WA FFU,WAANDAMANAJI IJUMAA



WAKATI Jeshi la Polisi Kanda Maalumu ya Dar es Salaam likizuia maandamano ya baadhi ya Waislamu yaliyotangazwa kufanyika Novemba mosi na mbili mwaka (kesho na keshokutwa)  kushinikiza kutolewa rumande kwa Katibu wa Jumuiya na Taasisi za Kiislamu Tanzania, Sheikh Issa Ponda, ujumbe mfupi   wa simukuhamasisha maandamano hayo unazidi kusambazwa kwa waisilamu maeneo mbalimbali.
Raha za Pwani imefanikiwa kunasa meseji hiyo ikieleza kwamba siku hiyo shule zote za Kisilamu  zitafungwa ilikutoa fursa kwa wanafunzi walimu na wazazi wa kisilamu nao kushhiriki kwenda kwenye mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kushindikiza kutolewa kwa sheikh Ponda  ambapo siku ya pili yake (Ijumaa) kufanya maandamano makubwa jijini Dar es Salaam.

Kamanda wa Polisi wa Kanda Maalumu ya Dar es Salaam, Suleiman Kova, alisema juzi kuwa maandamano hayo ni batili kutokana na kutopewa baraka na jeshi hilo. Alisema polisi imejipanga kuwashughulikia wote watakaofanya maandamano katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu.
Aidha, alisema Jeshi la Polisi linamsaka mtu anayechapisha vipeperushi vya kuchochea maandamano ambayo ni hatari kwa wananchi. Aliwataka wananchi kuendelea na shughuli za kiuchumi kutokana na kuimarishwa kwa usalama katika siku hizo ambazo watu hao wanataka kuandamana kinyume cha sheria.

“Hatutarudi nyuma kwa wale ambao watavunja sheria na kuvuruga amani ya nchi katika siku hizo mbili,” alisema Kova.
Kova alisema haki itapatikana mahakamani, hivyo hakuna haja ya kufanya maandamano katika mahakama hiyo ambayo inasikiliza kesi ya kiongozi huyo

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE