WASHAMBA WA USAFIRI WA TRENI DAR WAGOMA KUTEREMKA MWISHO WA SAFARI

Wakazi wa Dar es Salaam ambao hawajawahi kupanda treni, leo wameonesha maajabu ama ushamba baada ya kupanda Treni ya Kati TRL, na kugeuka watalii kwa kulipa nauli moja na kuamua kutoteremka mwisho wa safari na kuamua kugeuka nalo kwa lengo la kutalii.

Kitendo hicho cha abiria hao washamba wa treni, kimesababisha baadhi ya abiria waliokuwa wakisubiri huduma hiyo usiku kwenye Stesheni ya TRL mjini kukosa nafasi, baada ya mabehewa yote kujaa wao.

Abiria wengi waliokosa usafiri huo katika stesheni hiyo walionekana kukerwa na kitendo hicho huku wengine wakiwakaripia abiria waligoma kuremka kuwapisha.

Baadhi ya waliokosa safari hiyo waliamua kwa hasira kuondoka na kwenda kwenye vituo vya daladala kurudi makwao jana saa mbili usiku.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE