JK ASHINDA KWA KISHINDO UENYEKITI CCM TAIFA, DK. SHEIN AWA MAKAMU MWENYEKITI CCM VISIWANI NA MANGULA MAKAMU MWENYEKITI BARA

 Rais Jakaya Kikwete ameshinda tena uenyekiti wa chama hicho kwa kupigiwa kura 2395 katika uchaguzi uliofanyika leo kwenye ukumbi wa Kizota, Dodoma.


                                           Mwenyekiti  mpya wa CCM, Rais Jakaya Kikwete
                          Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Visiwani, Dk. Ali Mohamed Shein
 Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Bara, Philip Mangula


NA RICHARD MWAIKENDA Wajumbe waliopiga kura ni 2397, waliompigia kura Jakaya Kikwete ni 2395, wawili walipiga kura za hapana na hakuna kura zilizoharibika, hivyo Kikwete atakiongoza chama hicho kwa muda wa miaka mitano hadi 2017.

Msimamizi wa Uchaguzi huo, Spika Anne Makinda ametangaza matokeo ya uchaguzi  huo, ambapo Makamu Mwenyekiti wa CCM Tanzania Visiwani, Dk. Ali Mohamed Shein ameshinda kwa asilimia mia kwa kupata kura  zote zilizopigwa 2397 na Makamu Mwenyekiti Tanzania Bara, Philip Mangula naye amepita na kushinda nafasi hiyo kwa kupata kura zote 2397.

Wajumbe 10 wa NEC waliofanikiwa kupenya kwenye uchaguzi huo Tanzania Bara ni Steven Wasra, 2135, January Makamba 2093, Mwigulu Mchemba 2012, Martine Shigella 1824, William Lukuvi 1805,Bernad Membe 1455, David Mathayo 1414, Willsom Mukama 1374, Jackson Msome 1207 na Fenella Mkangala..

Kwa upande wa Zanzibar wajumbe ni, Makame Mbarawa, Mohamed Seif Khatib, Yusufu Omary Mzee, Shamsi Vuai Nahodha, Samia Suluhu Hassan. na wengine.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.