KUSIKO NA USIMAMIZI WA SHERIA NYAMA PORI NI HADHARANI KAMA HIVI
Mkazi
wa Kijiji kimoja kilichomo katika Wilaya ya Muleba Mkoani Kagera,
akisafirisha Nyama ya Wanyama Pori, ambayo haikuweza kufahamika kwa hara
ni nyama ya mnyama gani, ambapo muda mchache kabla ya jamaa huyu eneo
hili walipita wengine wawili wakiwa wameongozana huku pia wakiwa
wamebeba nyama kama hii, ambayo imeelezwa hupelekwa kuuzwa kijiji cha
mbele ambako kumechangamka kutokana na mabasi mengi kusimama maeneo hayo
ambayo jamaa hawa hufanya biashara ya kuchoma nyama hii.
Hivyo
wasafiri kueni makini kula hovyo nyama za kuchoma njiani msizozijua kwa
haraka kwani unaweza kula usichokitarajia na pia usafirishaji huu na
uwindaji haramu kama huu huendelea katika maeneo kama haya kutokana na
wasimamizi wa sheria zilizowekwa kuwa wakifanyika kazi zao mojini tu
bila kufika katika maeneo husika.
Comments