Shirikisho la Ngumi la Kimataifa (IBF) katika bara la Afrika, Ghuba ya
Uajemi na Mashariki ya Kati limemtamngaza bwana Lucas Rutainurwa wa kampuni ya
Kitwe General Traders ya jijini Dar-Es-Salam kama Promota wa mwaka 2012.
Akitangaza habari hizi, Rais wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba ya
Uajemi na Mashariki ya Kati Mtanzania Onesmo Ngowi alisema kuwa bwana Lucas
Rutainurwa alifanikisha Watanzania wawili kuwa mabingwa wa IBF katika bara
la Afrika, Ghuba ya Uajemi an Mashariki ya Kati mwaka unaoishia Desemba 2012.
Katika harakati zake za kuipa Tanzania sura ya kimataifa katika
tasnia ya ngumi za kulipwa Rutainurwa na kampuni yake ya Kitwe General Traders
waliandaa mapambano makubwa mawili ambayo yalizidi maandalizi ya mapambano yote yaliyowahi
kufanyika Tanzania kwa miaka ya karibuni.
Mwezi
April mwaka 2012, Rutainurwa na Kitwe General Traders waliandaa pambano
lililowakutanisha mabondia Francis Cheka na Mada Maugo wote wa Tanzania
kugombea mkanda wa IBF bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya
Kati katika ukumbi wa PTA jijini Dar-Es-Salaam. Katika mpambano
huo bondia Francis Cheka aliibuka kidedea baada ya kumsimamisha Maugo
katika raundi
ya nane.
Francis Cheka alitetea vyema mkanda wake huo tarehe 26 Desemba jijini
Arusha alishinda kwwa points bondia Chimwemwe Chiotcha kutoka nchini Malawi katika pambano lao la raundi 12.
Mwezi wa nane mwaka 2012, Rutainurwa na Kitwe General Traders
waliandaa mpambano mwingine kati ya bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania na
Sunday Kizito kutoka Uganda kugombea mkanda wa IBF katika bara la Afrika, Ghuba
ya Uajemi na Mashariki ya Kati katika uzito wa Unyoya (Featherweight).
Katika mpambano huo bondia Ramadhani Shauri wa Tanzania alimsimamisha
Sunday Kizito kutoka Uganda katika raundi ya 9 na kutangazwa kuwa bingwa mpya
wa IBF.
Kupatikana
kwa mabingwa hao, kumeifanya Tanzania kuwa nyumbani kwa
mabingwa wawili wa IBF na hivyo kuiweka nchi hii katika ngazi moja na
chache duniani hususa katika bara la Afrika zikiwemo Afrika ya
Kusini, Ghana, Morocco, Algeria na Cameron.
Shirikisho
la Ngumi la Kimataifa lina makao yake makuu yanayoratibu
bara la Afrika, Ghuba ya Uajemi na Mashariki ya Kati kutokea katika jiji
la Dar-Es-Salaam, Tanzania. Hii ni heshima ya kipekee kwa nchi ya
Tanzania kwani nchi nyingi zinagombania kuwa makao makuu ya shirikisho
hii kubwa kuliko yote duniani.
IBF imemshukuru sana bwana Lucas Rutainurwa na kampuni yake ya Kitwe
General Traders kwa mafanikio haya mazuri.
Bwana Lucas atapewa tuzo yake la kuwa promota wa mwaka wa IBF katika
bara la Afrika mwaka 2012 rasmi wakati wa mkutano wa 30 wa IBF/USBA utakaofanyika
katika jiji la Berlin, nchini Ujerumani Mai mwakani.
Katika hatua nyingine:
Bwama Michael Tetteh na bwana Henry Many-Spain wa GoldMike Promotions and
Golden Concept za jiji la Accra, Ghana wameteuliwa kama promota wa mwaka 2012
wa mapambano ya IBF ya mabara. Bwana Tetteh amepromoti mapambano mengi ya IBF
ya mabara (Continental Titles) kuliko promota mwingine yeyote katika bara la Afrika.
Aidha, IBF imemteua bwana
Branco Milenkovik wa kampuni ya Branco Sports Productions ya jiji la Johannesburg,
nchini Afrika ya Kusini kama promota wake wa mwaka wa mapambano ya dunia mwaka
2012. Hii ni mara ya 3 mfululizo kwa Branco kuteuliwa kama promota wa mwaka kwa
kuandaa mapambano mengi ya IBF ya ubingwa wa dunia.
Imetolewa na:
Makao makuu
IBF/Africa
Dar-Es-Salaam
Comments