Bango likionesha idadi ya Watanzania wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi uliofanywa na Rais Jakaya Kikwete leo kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam.
Rais Jakaya Kikwete akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Idadi ya Watanzania kwa sasa ni 44,929,002. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kikundi cha uhamasishaji kutoka wilayani Temeke, kikishangilia kwa furaha wakati wa uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa hafla hiyo
Rais Jakaya Kikwete (kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi wakicheka kwa furaha baada ya uzinduzi huo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kamishina wa Sensa, akipongezwa na viongozi wa serikali kwa kufanikisha sensa hiyo
Baadhi ya viongozi wa vyama na serikali wakiwa katika hafla hiyo
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani akihutubia wakati wa hafla hiyo
Sasa ni wakati wa kuimba utenzi wa kusifu sensa hiyo
Wanahabari wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Traiphone Mweji, Adamu Gire, Chris Mfinanga na Antony Siame.
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakishangilia huku wakiwa na mabango ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa na viongozi wengine wa Serikali pamoja na watumishi wa Ofisi za Taifa za Takwimu za Tanzania Bara na visiwani wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Rais Jakaya Kikwete akiteta na Mwenyekiti wa Taifa wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba wakati wa hafla hiyo.
Rais Jakaya Kikwete akibofya kwenye kompyuta kuzindua rasmi matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam. Idadi ya Watanzania kwa sasa ni 44,929,002. PICHA NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kikundi cha uhamasishaji kutoka wilayani Temeke, kikishangilia kwa furaha wakati wa uzinduzi huo.
Rais Jakaya Kikwete akihutubia wakati wa hafla hiyo
Rais Jakaya Kikwete (kulia), Waziri Mkuu, Mizengo Pinda (katikati) na Mwenyekiti wa Kampuni za IPP, Reginald Mengi wakicheka kwa furaha baada ya uzinduzi huo. PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG
Kamishina wa Sensa, akipongezwa na viongozi wa serikali kwa kufanikisha sensa hiyo
Baadhi ya viongozi wa vyama na serikali wakiwa katika hafla hiyo
Mwakilishi wa Umoja wa Mataifa wa Shirika la Idadi ya Watu Duniani akihutubia wakati wa hafla hiyo
Sasa ni wakati wa kuimba utenzi wa kusifu sensa hiyo
Wanahabari wakijadiliana jambo wakati wa uzinduzi huo. Kutoka kushoto ni Traiphone Mweji, Adamu Gire, Chris Mfinanga na Antony Siame.
Baadhi ya wakazi wa Dar es Salaam wakishangilia huku wakiwa na mabango ya kumpongeza Rais Jakaya Kikwete.
Rais Jakaya Kikwete (katikati waliokaa) akiwa na viongozi wengine wa Serikali pamoja na watumishi wa Ofisi za Taifa za Takwimu za Tanzania Bara na visiwani wakati wa uzinduzi wa matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi kwenye viwanja vya Mnazi Mmoja, Dar es Salaam
Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba akimpongeza Rais Kikwete kwa kufanikisha sensa hiyo |
HOTUBA YA MHESHIMIWA JAKAYA MRISHO KIKWETE,
RAIS WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA,
KWENYE UZINDUZI WA MATOKEO YA AWALI YA
SENSA YA WATU NA MAKAZI YA MWAKA 2012,
VIWANJA VYA MNAZI MMOJA, DAR ES SALAAM
TAREHE 31 DESEMBA, 2012
Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal,
Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania;
Mheshimiwa Balozi Seif Idd, Makamu wa
Pili wa
Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar;
Waheshimiwa Mawaziri;
Waheshimiwa Mabalozi;
Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa;
Viongozi
na watendaji wakuu wa Serikali;
Viongozi
wa Vyama vya Siasa, Viongozi wa Dini, Viongozi wa Jamii; Wanahabari;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana;
Nashukuru kwa kunialika kuja kushiriki kwenye
tukio hili muhimu na la kihistoria la kutangaza matokeo ya awali ya Sensa ya
Watu na Makazi ya Mwaka 2012. Haya ni matokeo ya kazi ya kuhesabu watu
iliyofanyika kwa siku 14 kuanzia tarehe 26 Agosti, 2012 hadi 4 Septemba, 2012.
Ndugu wananchi;
Napenda
kutumia nafasi hii kutoa pongezi za dhati kwa wale wote waliofanikisha zoezi la
kuhesabu watu na wale waliokamilisha uchambuzi unaotuwezesha leo kutangaza
idadi ya Watanzania ilivyo sasa. Kwanza
kabisa napenda kutambua Kamati ya Taifa ya Sensa iliyoongozwa na Mheshimiwa
Mizengo Peter Kayanza Pinda, Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania akiwa na Mheshimiwa Balozi Seif Ali Idi,
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar akiwa Mwenyekiti upande wa Zanzibar. Nawashukuru kwa uongozi wao mzuri ambao
matunda yake ndiyo haya yanayotukusanya leo.
Pia nawashukuru wajumbe wa Kamati za Sensa za Mikoa na Wilaya nchini.
Pili, napenda kuwatambua viongozi na
wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Takwimu ya Jamhuri ya Muungano chini ya
uongozi wa Mama Albina Chuwa na wenzao wa Afisi ya Mtakwimu Mkuu wa Zanzibar chini ya uongozi
wa Ndugu Mohammed Hafidh Rajab.
Nawapongeza kwa umahiri wao katika kuongoza, kuratibu na kisimamia utekelezaji
wa jukumu lenyewe la kuhesabu watu. Ni
wao kuliko mtu mwingine ye yote ndiyo waliokabidhiwa kazi ngumu ya kutengeneza
mipango na taratibu za kufanya zoezi lenyewe.
Walitayarisha madodoso, kuyachapisha, kuyasambaza, kuteua watu wa
kuhesabu watu na wasimamizi wao.
Waliwafundisha wajibu wao na kuwasimamia katika utekelezaji wao. Ni wao pia waliohakikisha kuwa madodoso yote
yanakusanywa na uchambuzi unafanywa mpaka sasa tuko tayari kutangaza matokeo.
Nawatambua
na kuwashukuru makarani wa sensa waliopita nyumba kwa nyumba kuhesabu watu na
kukusanya taarifa mbalimbali kwa mujibu wa madodoso waliyokuwa nayo. Tunatoa shukrani na pongezi maalum kwao kwa
sababu ni wao hasa waliowezesha kupatikana taarifa itakayotangazwa leo na
nyingine zitakazofuatia siku za usoni. Kama si wao tusingekusanyika hapa leo.
Nawapongeza kwa umakini wao na moyo wao wa uvumilivu na uzalendo. Haikuwa kazi rahisi kwa ukubwa wa kazi
yenyewe. Pia, walikumbana na changamoto
mbalimbali ikiwa ni pamoja na baadhi ya maeneo kuwa na mazingira magumu ya
kufanyia kazi kama vile ya usafiri. Lakini pia
kulikuwa na ugumu wa kupata taarifa kutoka kwa wanaoulizwa. Baadhi hawakutoa ushirikiano
unaotakiwa. Yalikuwepo pia matatizo ya
kupata huduma stahiki za kufanyia kazi na hasa posho. Nafahamu kuwa wapo bado wanaodai stahili zao. Hazina wamekiri hilo na kuahidi watalimaliza haraka.
Ndugu
wananchi;
Kufanya sensa ni kazi kubwa na ghali sana. Hata hivyo nchi zote duniani hufanya sensa
kwa sababu ya umuhimu wake. Kupitia
Sensa, hupatikana taarifa muhimu za kutumiwa na Serikali kupanga mipango ya
maendeleo ya nchi na jinsi ya kuhudumia wananchi. Taarifa hizo hutumika na wadau mbalimbali
katika shughuli zao za kuwahudumia wanadamu.
Ndiyo maana madodoso yalikuwa na mambo mengi na ndiyo maana tumeambiwa
kuwa taarifa ya leo ni ya mwanzo tu.
Zipo taarifa zitakazofuatia zenye uchambuzi wa mambo mbalimbali. Naomba tuwe na subira kwa taarifa mbalimbali tunazozitaka, kwani tutazipata
wakati wake utakapofika. Kwa niaba yenu
niwaombe wahusika wafanye kila wawezalo kuhakikisha kuwa taarifa hizo
zinapatikana kwa wakati uliopangwa.
Ndugu
Wananchi;
Nitakuwa mwizi wa fadhila kama
sitawatambua watu wengine wafuatao: Wa kwanza ni Hajat Amina Mrisho,
Kamishna wa Sensa ambaye tulimkabidhi jukumu la kutoa uongozi wa kisiasa katika
kazi ya kuhesabu watu na kuwa kiungo kati ya wataalamu na uongozi wa
Serikali. Vile vile, tulimpa kazi ya kusaidia
kufikisha ujumbe pande zote ili kuona kuwa mambo yanakwenda vizuri. Bahati nzuri mwenyewe ni mjuzi wa masuala ya
takwimu. Alitokea huko kabla ya
kumchukua na kumleta katika shughuli za uongozi wa kisiasa. Hivyo, kazi ilikuwa mikononi kwa mwenyewe. Namshukuru kwa kuifanya kazi hiyo kwa ufanisi
mkubwa. Anao mchango mkubwa katika
mafanikio haya. Wa pili ni wananchi wa Tanzania. Nawashukuru kwa ushirikiano wao. Kabla na wakati wa Sensa, kulikuwa na purukushani
na maneno mengi ya upotoshaji na kutishia kuvuruga zoezi lenyewe. Wapo wenzetu walioamua kuendesha kampeni ya
kutaka watu wasusie. Wapo walioamua
kufanya maandamano na mikutano ya siasa wakati huo na jitihada zote za kuwasihi
wasubiri siku 14 zipite walizipuuza.
Wakati mwingine unashindwa kuelewa baadhi yetu tuna dhamira gani katika kujihusisha
na shughuli za siasa? Hivi inakuwaje washindwe kutambua umuhimu wa kuhakikisha
jambo kubwa kama hili linafanikiwa? Hivi zoezi
la sensa lisipofanikiwa kiongozi wa siasa au wa dini unanufaika nini? Ndiyo maana nawashukuru sana wananchi kwa ushirikiano wao uliofanya
njama za kuvuruga zoezi kushindwa.
Ndugu
wananchi;
Wa
tatu
ni Wajumbe wa Kamati za Sensa za Mikoa na Wilaya kwa kufanikisha zoezi la Sensa
katika Mikoa na Wilaya zao. Nawashukuru Wakuu wa Mikoa na Wilaya wote nchini
kwa uongozi wao mzuri. Wa nne ni viongozi wa kijamii wakiwemo wa vyama vya
siasa, madhehebu ya dini na wa kimila waliosimama kidete kuhamasisha wafuasi
wao kushiriki katika zoezi la Sensa ya Watu na Makazi. Tunawashukuru kwa mchango
wao muhimu. Wa tano ni wamiliki wa vyombo vya habari na wana habari. Nawashukuru kwa kufanya kazi kubwa na nzuri
ya kuhamasisha na kuelimisha jamii katika kipindi chote cha utekelezaji wa
zoezi la Sensa. Wito wangu kwenu ni kwamba, endeleeni kuelimisha na kuhamasisha matumizi ya taarifa za Sensa kwa
maendeleo ya taifa letu.
Wa
mwisho, lakini siyo kwa umuhimu, nawashukuru sana washirika wetu
wa maendeleo wakiwemo UNFPA, DFID, JICA, CIDA na Benki ya Dunia kwa mchango na
msaada wao mkubwa. Nawashukuru Wenzetu hawa wametupa ushirikiano mkubwa uliotuwezesha
kufanikisha zoezi la Sensa hadi kufikia hatua hii ya sasa ya kutoa matokeo ya
awali. Naomba washirika wetu wa
maendeleo waendelee kushirikiana nasi kukamilisha kazi hii na pia katika
kuimarisha sekta ya takwimu nchini.
Ndugu
wananchi;
Baada ya kusema maneno hayo sasa nipo tayari kuzindua
rasmi matokeo ya awali ya Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012. Kwa heshima na unyeyekevu mkubwa natangaza
kuwa kwa mujibu wa Sensa ya Watu na Makazi iliyofanyika kwa siku 14 kuanzia
Agosti 26, 2012, Tanzania ina watu 44,929,002
ambapo Tanzania Bara kuna watu 43,625,434 na Zanzibar kuna watu 1,303,568.
Katika Sensa ya tatu ya mwaka 2002 tulikuwa milioni 34.4 hivyo tumeongezeka kwa watu milioni 10.5 ongezeko ambalo ni sawa na asilimia 2.6 kwa mwaka.
Naomba taarifa hizi zitumike kwa madhumuni yaliyokusudiwa ambayo ni
kuboresha maisha ya kila Mtanzania.
Ndugu
Zangu;
Hii ni Sensa ya nne kufanyika nchini tangu
kuasisiwa kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania mwaka 1964. Sensa ya kwanza ilifanyika mwaka 1967 ambapo
nchi yetu ilikuwa na watu 12,313,054. Tanzania Bara ilikuwa na watu 11,958,654 na Zanzibar watu 354,400. Kwa maana hiyo, katika miaka 45 tangu Sensa ya kwanza na hii,
Watanzania wameongezeka kwa watu milioni
33.
Ndugu
Wananchi;
Kama kasi ya ongezeko la watu la asilimia 2.6 halitapungua ifikapo mwaka
2016 nchi yetu itakuwa na watu milioni 51.6.
Inawezekana idadi hiyo ikaonekana kuwa siyo tatizo la kuumiza kichwa kwa
nchi kubwa kama yetu, lakini ni mzigo mkubwa kwa taifa, jamii na uchumi kuwahudumia. Inabidi pawepo na mikakati madhubuti na
ionekane katika mipango ya maendeleo kuanzia sasa jinsi ya kuhudumia watu hao 51.6 na zaidi ya hao miaka
inayofuata. Kwa familia, lazima tutambue
umuhimu wa kupanga uzazi, vinginevyo hali ya maisha itashuka sana. Kwa ujumla hatuna budi kufanya kazi kwa bidii
zaidi na nguvu zaidi.
Asanteni sana kwa kunisikiliza.
Comments