RAIS KIKWETE AKAGUA UKUMBI WA KISASA WA MIKUTANO WA KIMATAIFA JIJINI DAR ES SALAAM
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akikagua ukumbi mkubwa wa mikutano multi-purpose conference Hall' uliopo mtaa wa Shaaban Robert jijini Dar es Salaam. Ukumbi huo wa Serikali upo chini ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa. Ujenzi wa Ukumbi huo uko katika hatua za mwisho na Rais Kikwete mbali na kuridhishwa na hatua hiyo ametoa maelekezo kwa wahandisi kutenga sehemu maalumu kwa Wapiga picha na waandishi wa habari ili waweze kufanya kazi zao kwa ufanisi. Rais Kikwete pia ameelekeza wahandisi kuweka viti na meza zinazohamishika ili kukidhi matakwa ya mikutano na vikao vya aina mbalimbali (picha na Freddy Maro)
Comments