MANISPAA YA ILALA YATOA TAARIFA YA KUPOROMOKA KWA JENGO LA GHOROFA 16 DAR ES SALAAM



Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kulia), akizungumza na Madiwani wa Manispaa hiyo kwenye kikao cha dharura cha taarifa ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 na kuua watu 34 kilichoketi Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Meya, Kheri Kessy. (Picha habari na habari za jamii blog)
 Madiwani wa Manispaa hiyo wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Diwani Viti maalumu (CCM), Grace Shelukindo, Hajat Lai Ally na Diwani wa Kata ya Kivule Nyansika Motena.
 Mwenyekiti wa Kamati ya Mipango Mji wa Manispaa ya Ilala, Magina Lugungulo (kushoto), Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma za Jamii, Angelina Malembeka (katikati), wakimsiliza kwa makini Mwenyekiti wa Kamati ya Ujenzi Siltanb Ahamed Salim katika kikao hicho.
 Madiwani wa Manispaa hiyo wakiwa kwenye kikao hicho. Kutoka kushoto ni Diwani Viti maalumu (CCM), Grace Shelukindo, Hajat Lai Ally na Diwani wa Kata ya Kivule Nyansika Motena.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwendaaslala Maganga (kulia), akisoma taarifa hiyo. Kushoto ni Naibu Meya, Kheri Kessy na Mstahiki Meya Jerry Silaa.
 Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwendaaslala Maganga (kulia), akimkaribisha Mshahiki Meya kutoa taarifa hiyo hiyo. Kushoto ni Naibu Meya, Kheri Kessy na Mstahiki Meya Jerry Silaa.
 Mstahiki Meya Jerry Silaa (katikati), Naibu Meya Kheri Kessy (kushoto) na Mkurugenzi wa Manispaa ya Ilala, Mwendaaslala Maganga wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu wa ajali ya kuporomokewa na ghorofa hilo.
 Madiwani wakiwa wamesimama kwa dakika moja kuwakumbuka marehemu hao.
 Mstahiki Meya wa Manispaa ya Ilala, Jerry Silaa (kulia), akizungumza na Madiwani wa Manispaa hiyo kwenye kikao cha dharura cha taarifa ya kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 na kuua watu 34 kilichoketi Dar es Salaam leo. Kushoto ni Naibu Meya, Kheri Kessy. (Picha habari na habari za jamii blog)
 Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho.
 Madiwani wakiwa kwenye kikao hicho cha dharura.
 Diwani wa Kata ya Kiwalani, Saidi Kitambuliyo (kushoto), akiteta jambo na Diwani wa Viti Maalumu, Mwanaisha Mwita Siwani kwenye mkutano huo.

Na Dotto Mwaibale

MANISPAA ya Ilala imesema si mamlaka pekee ya kusimamia majenzi hivyo isitupiwe lawama kwa lolote kufuatia kuporomoka kwa jengo la ghorofa 16 mapema wiki iliyopita.

Hayo yamebainishwa na Mstahiki Meya wa Manispaa hiyo Jerry Silaa kwenye kikao cha dharura cha madiwani kilichoketi Dar es Salaam leo kupokea taarifa ya kuporomoka kwa jengo hilo lililokuwepo katika makutano ya barabara ya Morogoro na Mtaa wa Indira Ghandi katikati ya jiji la Dar es Salaam na kuua watu 34.

Alisema katika suala la majenzi kuna wadau mbalimbali wanahusika kusimamia majenzi kama sheria mbalimbali zinavyo ainisha.
"Tunaomba ileweke hivyo kwa umma kwamba halmashauri ya manispaa ya Ilala si mamlaka pekee ya usimamizi" alisema Silaa.
Aliongeza kuwa kazi kubwa inayofanywa na manispaa hiyo kumkubalia muuombaji kibali cha ujenzi, mkupitia michoro yake ambayo inakuwaq imeandaliwa na wasanifu na wakadiriaji majengo ambao wanasimamiwa na manispaa.

Alisema Halmashauri huwa haina nafasi zaidi ya kitalaamu ya kusimamia katika masuala makubwa hasa ya vyumba na kiwaqngo cha saruji inayotumika isipokuwa kufuatilia kama anajenga kama ambavyo alionesha katika michoro iliyopitishwa.

Silaa alisema kuna vyombo vilivyowekwa kusimamia sheria za majenzi kama bodi ya wakandarasi, bodi ya wasanifu majengo, bodi ya usajili wa wahandisi ambazo zipo kisheria.

Alisema bodi ya usajili wa wahandisi ni mamlaka iliyoanzishwa kisheria na baadhi ya majukumu yake ni kufuatilia na kusimamia shughuli na utendaji kazi wa wahandisi ikiwa ni pamoja na kampuni zinazofanya ya utalaalamu ushauri wa usimamizi wa miradi ya majenzi mijini.

Alisema bodi ya wasanifu majengo, wakadiraji majengo ni mamlaka iliyoanzishwa kisheria na majukumu yake ni kusimamia shughuli na utendaji kazi unaofanyika hapa nchini kwa madhumuni ya kujiridhisha na kuhakikisha kama kazi ya ujenzi inayofanyika inafanywa na mtu ambaye amesajiliwa na bodi na anazingatia taratibu, kanuni na sheria zote zinazisimamia ujenzi mijini.

Alisema sheria za kusimamia masuala ya ujenzi mijini zilitungwa kwa mara ya kwanza mwaka 1920 wakati wa utawala wa Mwingereza na kujulika kama sheria za miji.

Aliongeza kuwa sheria hizo zililenga kusimamia shughuli zote za majenzi mijini na kuwa msimamizi wa sheria hizo zilikuwa ni Mamlaka za Miji, Manispaa na jiji kwa wakati huo kwa sasa ni majiji na Manispaa ya Miji.

Katika kikao hicho Meya Silaa na madiwani hao walitumia fursa hiyo kuwakumbuka kwa dakika moja waliofariki katika tukio hilo na majeruhi waliopo hositalini kwa matibabu pamoja na kutoa shukurani za pongezi kwa Rais Jakaya Kikwete kwa ushirikiano wake mkubwa aliouonesha baada ya tukio hilo.

"Shukuruani nyingi zimuendee Rais wetu Jakaya Kikwete kwa moyo wa upendo aliouonesha na kuziagiza taasisi mbalimbali, mahospitali na majeshi ya ulinzi na usalama kushiriki katika uokoaji na yeye mwenyewe kufika eneo la tukio mara mbili na hospitali ya Taifa Muhimbili kuwajulia hali majeruhi ni jambo la kiungwana sana" alisema Silaa.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

CHAMA KIPYA CHA WALIMU WAMUOMBA RAIS SAMIA AINGILE KATI MAKATO YA WANACHAMA WAO

TOFAUTI YA WATU WA DAR NA WA MKOANI NI HUU

IBENGE: YANGA SC WATAFUZU HATUA YA ROBO FAINALI.

NILIYOYABAINI KATIKA TRENI YA SGR DAR ,MORO HADI DODOMA … KADOGOSA REKEBISHENI MAMBO HAYA MTANIKUMBUKA