KINANA,NAPE WAFANYA MAMBO WILAYANI MAKETE

Wanachama wa CCM, wakiuelekeza njia msafara wa Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (haupo pichani) ulipokuwa unakwenda kwenye shina la Singida kufanya nao mkutano, ikiwa ni sehemu ya ziara ya kikazi ya kuimarisha uhai wa chama hicho, katika Kata ya Tandala, wilayani Makete.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akihutubia katika mkutano uliofanyika Shina la CCCM la Singida, wilayani Makete leo.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akiuongoza msafara baada kutokaa kwenye mkutano katika Shina la CCM la Singida, wilayani Makete.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye  akizungumza na Balozi wa Shina la Posta , Kata ya Tandala, wilayani Makete jana wakati wa ziara ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama hicho katika Mkoa mpya wa Njombe.

Wananchi wa Kata ya Ukwama, wilayani Makete, wakishangilia wakati Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo, wilayani,
Makete, wakati wa ziara ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama hicho katika Mkoa mpya
wa Njombe.
Kikundi cha ngoma ya asili ya kabila la wanyakyusa ngoma ya Ing'oma wakitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Iniho, wilayani Makete leo jioni, wakati wa ziara ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama.
Kikundi cha ngoma ya asili ya kabila la wanyakyusa ngoma ya Ing'oma wakitumbuiza wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Iniho, wilayani Makete leo jioni, wakati wa ziara ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama.
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akihutubia mkutano wa hadhara eneo la Iniho, wilayani Makete leo
Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana, akimshangaa mwanachama wa CCM,Rambon Sanjwe (57), akiwa ambaye amevaa kinyago. Kada huyo alijiunga na CCM mwaka 1977.
Kinana akiwaongoza wanachama wapya kula kiapo cha utii cha chama hicho katika mkutano huo wa hadhara.
Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akipiga gita huku mwandishi wa habari wa gazeti la Jambo Leo, Said Mwishehe akisikiliza kwa makini baada ya mkutano huo.



Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI