Kinywaji cha Chilly Willy yamwaga vifaa kwa Taswa FC, Taswa Queens


 Meneja Masoko wa TSN Supermarket, Yohana Manoli (kushoto), akimkabidhi Mwenyekiti wa timu ya soka ya Chama cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), Majuto Omari, msaada wa vifaa vya michezo vyenye thamani ya sh. mil. 3, vilivyotolewa kupitia kinywaji cha kuongeza nguvu  cha Chilly Willy kwa ajili ya timu ya Taswa FC na timu ya Wanawake ya Taswa Queens, Dar es Salaam jana. Taswa FC inajiandaa kupepetana na timu ya mabondia wa kulipwa ya Boxers FC Jumapili Leaders Club. Anayeshuhudia ni Meneja Uhusiano wa kampuni hiyo, Meshack Nzowa. PICHA NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA

Dar es Salaam. Mei 17, 2013
Kinywaji maarufu cha kuongeza nguvu, Chilly Willy Energy Drink kimetoa msaada wa jezi  na mipira kwa timu ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC na timu ya Netiboli, Taswa Queens kwa ajili ya kutumika michezo yake mbali mbali.


Meneja Masoko wa Kampuni ya TSN Group kinachosambaza kinywaji cha Chilly Willy Yohana Manoli alikabidhi vifaa hivyo kwa mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary katika hafla fupi iliyopfanyika kwenye mgahawa wa Hadees uliopo katikati ya jiji la Dar es Salaam.

Manoli alisema kuwa sababu kubwa ya kukabidhi vifaa hivyo kwa Taswa SC ni kutambua mchango wa waandishi wa habari katika kuendeleza michezo nchini na hasa ukizingatia kuwa kinywaji cha Chilly Willy hakina kilevi na ni maalum kwa wanamichezo.


Meneja Uhusiano na Mawasiliano wa  TSN Group, Meshack Nzowah alisema kuwa kinywaji chao cha Chilly Willy kina ubora wa kimataifa na wanaamini kuwa wanamichezo na wanajamii wataanza kutumia kinywaji hicho katika shughuli mbalimbali.
“Chilly Willy ni kinywaji ambacho hakina kilevi, kina ubora wa kimataifa na kutokana na hilo, kampuni ya TSN Group ikaamua kukisambaza nchini kwa lengo la kutoa bidhaa iliyobora zaidi, tunaamini wanamichezo wataanza kutumia hiki na vile vile ni maalum kwa waandishi wa habari na wadau wengine nchini,” alisema Nzowah.


Mwenyekiti wa Taswa SC, Majuto Omary aliipongeza kampuni inayosambaza kinywaji cha Chilly Willy na kuwaomba waandishi wa habari kuanza kutumia kinywaji hicho. Majuto alisema kuwa Chilly Willy imetambua mchango wa Taswa  SC katika kuendeleza michezo na kutoa msaada huo.


“Ni faraja kubwa kuwa na kinywaji hiki hapa nchini na hasa kwa kutujali wana habari, kwa vifaa hivi, Taswa FC na Taswa Queens zitakuwa na nguvu na ubora kama wa Chilly Willy,” alisema Majuto.


Majuto alisema kuwa jezi hizo watazizindua rasmi Jumapili katika mechi dhidi ya timu ya kombaini ya mabondia wa ngumi za kulipwa nchini itakayochezwa kwenye uwanja wa Leaders Club kuanzia saa 5.00 asubuhi.


Alisema kuwa timu ya mabondia itaongozwa na bondia mkongwe nchini, Rashid “Snake Man” Matumla na mabondia wakali wengine kama Francis “SMG” Cheka, Cosmass  Cheka, Mbwana Matumla, Karama Nyilawila, Maliki Kinyogoli, Hassan Matumla, Daudi Mhunzi, Saidi Yazidu, Francis Miyeyusho , Thomas Mashali, Charles Mashali na wengine wengi.
Mwisho….

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA