BARAZA LA MADIWANI KILOLO LAAGIZA WAUGUZI WANAO KODISHA AMBULENCE NA KUPOKEA POSHO KWA MGONJWA HOSPITAL TEULE YA ILULA KUCHUNGUZWA ........
Madiwani wakimkumbuka aliyekuwa mkurugenzi wa Kilolo na diwani wa kata ya Ukumbi
Diwani mteule wa kata ya Ng'ang'ange wilaya ya Kilolo Msuva (kushoto) akila kiapo mbele ya mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo Joseph Muhumba leo anayeshudia wa pili kulia ni kaimu mkurugenzi wa Halmashauri ya Kilolo Benson Kilange
Mbunge wa jimbo la Kilolo Prof Peter Msolla kulia akishuhudia zoezi la kuapishwa diwani mteule wa kata ya Ng'ang'ange leo
Kiapo cha utii kwa diwani mteule
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Kilolo JOseph Muhumba akifungua kikao cha baraza la madiwani leo
BARAZA la madiwani katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilolo mkoani Iringa limeagiza kufuatilia tuhuma zilizotolewa na mmoja kati ya madiwani wa baraza hilo kuhusiana na Hospital teule ya Ilula Ilula kuwakodisha gari la wagonjwa (Ambulence) wagonjwa wanaopewa rufaa kwenda Hospital ya mkoa pamoja na kuomba posho ya Tsh 10000 kwa mgonjwa .
Hatua hiyo imekuja kufuatia madai yaliyotolewa na diwani Anna Kulanga kuhusiana na mwenendo usiofaa unaofanywa na uongozi wa Hospital hiyo teule ya Ilula kwa kuwakodisha Ambulence wagonjwa.
Diwani Kulanga alisema kuwa hatua iliyofikiwa katika Hospital hiyo si nzuri kwani siku za hivi karibuni walipata kukodisha Ambulence hiyo kwa majeruhi wa ajali ambae alitakiwa kukimbizwa katika Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Iringa ila mbali ya majeruhi huyo kupoteza maisha njiani ila bado wauguzi wawili waliomsindikiza majeruhi huyo walitaka ndugu kulipa gharama ya Ambulence kiasi cha Tsh 40000 pamoja na kuwalipa posho ya Tsh 20000 wauguzi wawili walioongozana na majeruhi huyo.
Comments