WAZIRI MKUU PINDA AHIMIZA KUTUMIA TOVUTI KUU YA SERIKALI NA MKONGO WA TAIFA


NA MAGRETH KINABO – MAELEZO
WAZIRI  Mkuu Mizengo Pinda amewatoa wito kwa vyuo vikuu , taasisi za serikali, benki  na jamii  kutumia Tovuti   Kuu ya Serikali na Mkongo wa Taifa wa Mawasiliano katika kupata huduma mbalimbali za serikali ili   kurahisisha  mawasiliano kwa gharama nafuu.
Kauli hiyo imetolewa jana jioni na Waziri Mkuu, mheshimiwa  Pinda wakati akizindua Tovuti Kuu ya Serikali katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius K. Nyerere  jijini Dares Salaam mara baada ya  kutembelea   ofisi ya Wakala ya Serikali  Mtandao (eGA) na Mkongo wa Taifa.
 Akizungumzia kuhusu tovuti hiyo Waziri Mkuu Pinda alisema kitu muhimu ambacho mtu yoyote kuweza kupata taarifa  anazozihitaji mfano vile masuala ya kilimo au  kuomba uraia wa Tanzania. Hivyo lengo lake ni kuisadia Serikali kufanya kazi kiutalaam.
“ Kwa hiyo ni mambo yanayoifanya nchi kwenda kwa wakati. Tumeanzisha matumizi ya  tovuti hii kwa  sababu mahitaji yake  katika soko ni makubwa,”  alisema  Waziri Mkuu Pinda.
 Akizungumzia kuhusu  mkongo huo alisema  moja ya changamoto iliyopo  matumizi yake  bado ni  madogo, kwani  yako  chini  ya asilimia tano , hivyo kuna umuhimu wa kuongeza kasi ya matumizi.
 Alisema  Serikali itaendelea  kukabiliana  na changamoto za kiusalama katika masuala hayo.
Kwa upande wake Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Celina Kombani aliwataka wanafunzi na vijana kubadili  mtazamo kwa kutumia mitandao ya kijamii kwa mambo yasiyofaa badala yake  watumie tovuti hiyo ili kuweza kuelewa  historia ya nchi ,sheria na mambo mengine  mbalimbali.
 Aliongeza  kuwa tovuti hiyo inarahisisha utoaji wa huduma za Serikali kwa wananchi , pia na kuongeza uwajibikaji.
 Kwa upande wake  Mtendaji Mkuu wa  wakala huo, Dk. Jabiri  Bakari  alisema ina sehemu sita ambazo ni wananchi, Serikali,Taifaletu, Biashara, Sekta muhimu na Mambo ya Nje.
  Aliishauri Serikali kuviwezesha vitengo vya mawasiliano vya Serikali ili kuviwezesha kuweka taarifa sahihi kwa wakati.
 Aidha Jabiri alisema katika wameshaanza kazi ya kuwezesha  taarifa muhimu za Serikali  kupatikana kwa njia ya simu na iko kwenye hatua nzuri.
Alizipongeza Ofisi mbalimbali zilizowesha uwepo wa tovuti hiyo, ambazo Ofisi ya Rais , Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Katibu Mkuu Kiongozi, Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kupitia Idara ya Habari –MAELEZO  na Kamati ya Bunge  ya Sheria ,Katiba na Utawala.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI