Bendi ya 'Sikinde' kutoa burudani ya nguvu leo Sinza, Meeda

Bendi ya Mlimani Park Orchestra almaarufu kama Sikinde inategemea kuburudisha wapenzi wa muziki wa dansi kutoka Dar es Salaam leo Ijumaa (31 Januari 2014) katika ukumbi wa Meeda Sinza wilayani Kinondoni.

Akizungumza kwa niaba ya bendi ya Sikinde, Katibu wa bendi hiyo Hamis Mirambo amesema “baada ya kukaa muda mrefu bila kufanya shoo yeyote katika wilaya ya Kinondoni ,bendi ya Sikinde sasa ipo tayari kuwakosha moyo za wapenzi wa muziki wa dansi katika wilaya hiyo pamoja na watu wa wilaya za  jirani.”

“Tunapenda kuwaalika wapenzi wote wa muziki wa dansi wasikose kuhudhuria shoo yetu ambayo itaanza ukumbini Meeda kuanzia saa mbili usiku,” alisema Mirambo.

Aliongeza, “Karibuni mpate kuburudika na nyimbo za zamani na mpya kutoka bendi hii kongwe hapa nchini. Mpate kusikia kutoka kwa msanii Bichuka na wengine wengi…karibuni sana!”

Kwa hivi sasa bendi hiyo ya Mlimani Park Orchestra inamalizia kukamilisha albamu yao mpya iitawayo “Jinamizi la talaka” ambayo inabeba nyimbo kama Kibogoyo, Deni ntalipa, Ng’ombe haelemewi nunduwe,Kukatika kwa dole gumba, Tabasamu na Mkwezi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI