JUST IN:MWENYEKITI WA CHADEMA,MH. MBOWE, MH. HALIMA MDEE NA MH. PETER MSIGWA WASHIKILIWA NA JESHI LA POLISI MKOANI IRINGA
Akizungumza
kwa njia ya simu Ripota wa Mtandao huu, alisema kuwa, Viongozi hao wa
Chadema, wamekamatwa na Polisi leo asubuhi na kuwashikilia kwa muda
kituoni hapo wakihojiwa baada ya jana kupitisha muda katika mkutano wao
waliofanya mkoani hapo.
Aidha
imeelezwa kuwa viongozi hao walichelewa kufika eneo la mkutano baada ya
Rubani wao kupotea angani na kufika eneo hilo zikiwa zimebaki dakika
chache kabla ya muda wa mkutano kumalizika, jambo lililomfanya
mwenyekiti huyo kuwaomba Polisi wasimamizi wa usalama kuongea japo kwa
dakika chahe ili kuwajulisha wanachama wao kilichotokea.
Baada
ya kuruhusiwa kufanya hivyo imedaiwa kuwa mwenyekiti huyo aliyekuwa
ameongozana na wabunge wake wawili, alipitisha muda na kuzua maswali
miongoni mwa wanausalama wa mkoa huo, jambo lililowapelekea kukamatwa na
kuhojiwa kwa muda kituo cha Kati mkoani Iringa leo majira ya saa tatu
asubuhi na baadaye kuachiwa wakaendelea na safari zao.
Comments