SERIKALI YAWATOLEA UVIVU MAJANGILI, YANUNUA BUNDUKI 5,000 AINA YA AK47 KUKABILIANA NAO.


DAR ES SALAAM. 

SIKU moja baada ya Tanzania kutajwa na Shirika la Polisi la Kimataifa (Interpol) kuwa kinara wa biashara ya meno ya tembo Afrika Mashariki, Serikali imelipia kodi na kukabidhiwa bunduki 500 aina ya AK47 ili kukabiliana na ujangili katika hifadhi na mapori ya akiba nchini.
Waziri wa Maliasili na Utalii, Lazaro Nyalandu alisema jana kuwa silaha hizo zilizokuwa chini ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), tangu Novemba 2012 kutokana na kutokulipiwa kodi, zitasambazwa Ngorongoro, Selous, pamoja na Hifadhi za Taifa za Tanapa.


Kati ya silaha hizo, 250 zitapelekwa Idara ya Wanyamapori, 200 Tanapa na 50 Mamlaka ya Hifadhi Ngorongoro.


“Silaha hizi jumla ya Sh427 milioni kuzinunua lakini zilikwama TRA kwa sababu ya kutolipiwa kodi na ushuru mbalimbali, hivyo wizara yangu leo inatoa Sh212 milioni kwa ajili ya malipo hayo,” alisema Waziri Nyalandu.


Alisema silaha hizo zimekombolewa ikiwa sehemu ya kutekeleza maazimio ya Bunge na ahadi ya Serikali kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Maliasili, Ardhi na Mazingira.


Akizungumzia sababu za kuchelewa TRA, Nyalandu alisema kulikuwa na ubishi wa ama zilipaswa kulipiwa kodi au la, lakini mamlaka hiyo ilifafanua kuwa hayo ndiyo matakwa ya sheria, hivyo akaamua kutoa fedha hizo.


Alipoulizwa ni jinsi gani Serikali itadhibiti silaha hizo, Nyalandu alisema wizara yake inaandaa miiko ya matumizi yake ikiwamo kufuatilia makabidhiano yake na askari wanaokabidhiwa.


“Kumbuka hizi si silaha za kwanza kuwa nazo, tunazo nyingine za AK47 na hizo zimetuwezesha kukamata silaha haramu zaidi ya 2,000 zinazotumiwa na majangili,” alisema.


Silaha hizo zimepatikana ikiwa ni takriban wiki mbili tangu Rais Jakaya Kikwete abanwe na vyombo vya habari vya kimataifa akitakiwa kueleza mikakati iliyopo kupambana na ujangili ambao umeharibu sura ya Tanzania nje ya nchi.


Itakumbukwa kuwa miezi miwili iliyopita, Rais Jakaya Kikwete alilazimika kupangua Baraza la Mawaziri na kuwatimua mawaziri wanne kutokana na vitendo vya kinyama vilivyobainishwa na Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira wakati wa Operesheni Tokomeza Ujangili.


Majangili papa 40
Akijibu maswali ya waandishi wa habari, Waziri Nyalandu alisema majina ya majangili papa 40 ambayo Rais Kikwete alisema anayo, ‘yatabandikwa’ hivi karibuni. MWANANCHI

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MUSTAFA MKULO AFARIKI DUNIA

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI