KINANA, NAPE WAUNGURUMA BABATI MJINI LEO

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana akhutubia katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kwaraa, Mjini Babati, Mkoa wa Manyara jioni ya leo, akiwa katika mwendelezo wa ziara ya kuimarisha uhai wa chama, kukagua, kuhimiza na kusukuma ujenziwa miradi mbalimbali ya maendeleo inayotekelezwa kwa kufuata Ilani ya CCM, kukagua maandalizi ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa na kusikiliza kero za Wananchi na kuzitafutia ufumbuzi.
 Katibu  wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye, akihutubia katika mkutano  wa hadhara kwenye viwanja vya Kwaraa, Mjini Babati, Mkoa wa Manyara, ambapo alimshambulia Katibu Mkuu wa Chadema kwa kauli yake aliyoitoa hivi karibuni kuwa Umoja wa Mataifa umethibitisha kuwa hawana hati ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar ambapo alidai kuwa huo ni uongo wa dhahiri, hivyo wananchi wasiuamini asilani uongo huo.
 Kinana akiangalia ngoma ya asili alipowasili katika Kata ya Maisaka, wakati wa ziara yake Wilaya ya Babati Mjini.
 Kinana akiasaidiana na Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri kujenga jengo la Zahanati ya Malangi, katika Kata ya Maisaka, Babati.
 Kinana na Mbunge wa Babati Mjini, Kisyeri Chambiri wakitoka kukagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu katika Shule ya Komoto, Kata ya Bagara, Mjini Bbabati leo. Pia katika shule hiyo Kinana alikagua Hosteli, vyumba vya madarasa viwili na maabara.
 Kianana akipita kwenye shamba la mahindi na mbaazi baada ya kukagua ujenzi wa nyumba ya mwalimu wa Shule ya Sekondari Komoto, Jimbo la Babati Mjini leo.
 Kinana akipata maelezo kuhusu vifaa vilivyomo katika chumba cha maabara  alipotembelea ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara.
 Kinana akihutubia  baada ya kukagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Manyara, ambayo imeanza kutoa baadhi ya huduma za tiba.
 Kinana akizungumza  baada ya kukagua ujenzi wa Zahanati ya Nakwa, katika Kata ya Bagara, Babati Mjini.
 Wananchi wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana alipokuwa akizungumza nao baada ya kukagua mradi wa maji katika Kata ya Bonga, Babati Mjini.
 Kinana akimsikiliza Mbunge wa Jimbo la Babati Mjini, Kisyeri Chambili  akielezea jitihada alizozifanya kutoa fedha za kusaidia ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Shule ya Sekondari Sumaye, katika Kata ya Singe, Babati Mjini.
 Msafara wa Kinana ukielekea viwanja vya Kwaraa kwenye mkutano wa hadhara Babati Mjini.
 Nape akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kwaraa, Babati Mjini leo.
Kinana akihutubia katika mkutano wa hadhara kwenye viwanja vya Kwaraa, ambapo aliwataka viongozi wa kuteuliwa na kuchaguliwa kuwaheshimu wananchi kwa kusikiliza kero zao na kuzifanyia kazi, badala ya kuwadharau na kupora ardhi yao.PICHA ZOTE NA KAMANDA WA MATUKIO BLOG

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

Wasifu wa Kizza Besigye

KWA KHERI MAKARANGA UMEUTIMIZA MWENDO...

Kizza Besigye ‘akamatwa’ tena Uganda

KATI YA WATOTO 7 WA HAYATI MAGUFULI ANAYEJULIKANA ZAIDI NI JESCA

KIKOSI KILICHOITWA TAIFA STARS HIKI HAPA

UBORA UNAONEKANA: BENKI YA NMB YANG'ARA TUZO ZA EUROMONEY 2026

KIJANA WA KINYAKYUSA WA ENZI HIZO, NUSURA AMCHAPE WAZIRI MUONGO BUNGENI

WANAJESHI WAGOMA KWENDA IRAN KUPIGA