Taarifa Rasmi Kwa Umma Kutoka IKULU:Rais Jakaya Kikwete Alipowasili Toronto Canada kuhudhuria mkutano unaohusu Afya ya Mama na Mtoto kufuatia mualiko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mheshimiwa Stephen Harper.


 Rais Jakaya Kikwete
--
 Rais Jakaya Mrisho Kikwete amewasili Toronto Canada tarehe 27 Mei, 2014 usiku  kuhudhuria mkutano unaohusu Afya ya Mama na Mtoto kufuatia mualiko kutoka kwa Waziri Mkuu wa Canada Mheshimiwa Stephen Harper.

Mkutano wa Afya ya Mama na Mtoto , (Maternal, Newborn and Child Health -MNCH) unaanza Leo tarehe 28 – 30 Mei, 2014 ambapo Rais Kikwete pia anatarajiwa kuwa miongoni mwa wazungumzaji wakuu.

Lengo la mkutano huu ni kutoa nafasi kwa wataalamu na viongozi wa dunia kufikia makubaliano kwa pamoja kuhusu jitihada na hatma kuhusu MNCH.

Mkutano huu unatarajiwa kutilia mkazo jitihada za kuimarisha huduma za afya, kuweka kumbukumbu za taarifa, katika jitihada za kupunguza vifo vya mama na watoto wachanga katika nchi zinazoendelea.

Mkutano huu unatarajiwa kuhudhuriwa na kiongozi wa Kidini, Mhe. Aga Khan, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Bw. Ban Ki Moon na Bibi Melinda Gates , ambaye ni Mwenyekiti mwenza wa Taasisi ya Bill & Melinda Gates.

Wengine ni Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Afya Duniani (WHO) Bi. Margaret Chan na Bw. Antony Lake wa UNICEF.

Akiwa hapa Rais pia atakutana na wadau wa sekta ya biashara na uwekezaji wa Canada na Tanzania kabla ya kurejea Dar es Salaam.


Mwisho

Imetolewa na;
Premi Kibanga,
Mwandishi wa Habari wa Rais Msaidizi,
Toronto-Canada
28 Mei, 2014

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK MAGUFULI ATANGAZA KIAMA CHA MAJAMBAZI, WEZI NA MAFISADI KATIKA MIKUTANO YA KAMPENI SUMBAWANGA,TUNDUMA, ILEJE NA MBOZI

UWANJA WA NDEGE WA KIMATAIFA WA MSALATO DODOMA KUANZA KUTUMIKA SEPTEMBA 2026

BALOZI WA CHINA KUPITIA DKT. MAJULE APELEKA NEEMA KWA WANAWAKE DODOMA

IJUE HISTORIA YA PACOME ZOUZOUA

SERIKALI YAINGIA MAKUBALIANO YA USHIRIKIANO NA DIT KUIMARISHA USIMAMIZI WA MAAFA

BREAKING NEWS…!! SERENGETI BOYS WAVUNJA KAMBI NA VILIO KIBAO