WANARIADHA WAAHIDI KULETA HESHIMA KATIKA MASHINDANO YA JUMUIYA YA MADOLA NCHINI SCTOLAND

RTE1Baadhi ya wachezaji wa Tanzania wakiwa kwenye uwanja wa ndege wa Mwalimu J.K.Nyerere tayari kwa kupanda ndege kueleka nchini Scotland kwa ajili ya kushiriki mashindano ya jumuiya ya Madola.RTE3Na Frank Shija, WHVUM
Wanamichezo waahidi kuleta medali katika mashindano ya Olympic yanayotarajia kuanza tarehe 23 Julai jijini Glasgow Scotland.
Akizungumza mara baada ya kuwasili nchini jana wakitokea Ethiopia Kocha wa Timu ya Riadha aliyeambatana na wachezaji 8 Bw. Shaban Hiiti alisema kuwa ana imani kubwa na wachezaji wake walioteuliwa katika Timu ya Taifa kuwa watailetea heshima Taifa kwa kuwa mazoezi waliyoyapata wakiwa nchini Ethiopia yamewajengea uwezo mkubwa.

Hiiki aliongeza kuwa walipokuwa nchi Ethiopia kwa mazoezi wamejifunza mbinu mbalimbali kutokana na kuwa na program za kuwajengea uwezo wachezaji wake.
“Nimatumaini yangu wachezaji hawa walioteuliwa kujiunga na wenzao waliokuwa mazoezini katika nchini zingine ambapo wanamichezo wetu walienda kwa ajili ya mazoezi wataliletea Taifa letu heshima kubwa kwani wamepikwa wakapikika”. Alisema Kocha huyo.
Aidha kocha huyo amesema kuwa uwepo mazingira mazuri na vifaa bora vya mazoezi kumechangia kwa kiasi kikubwa kuinua ubora wa wanariadha hao ambao wamefanya mazoezi kwa takribani miezi miwili nchini Ethiopia.
Kwa upande wake mmoja wa wanariadha ambaye amebahatika kuitwa kwenye kikosi kitakachoshiriki mashindano hayo Bw. Alphonce Felix amesema kuwa anajisikia faraja kuwa miongoni mwa wanamichezo watakao iwakilisha nchi katika mashindano ya Olympic kupitia mchezo wa riadha.
Alphonce amesema kuwa atatumia ujuzi alioupata nchini Ethiopia walipokuwa wameweka kambi kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo.
Jumla ya wanariadha 9 na kocha wao waliweka kambi nchini Ethiopia ikiwa ni jitihada zinazofanywa na Serikali za kukuza na kuendeleza Sekta ya Michezo nchini kupitia mpango wa Diplomasia ya Michezo, ambapo wanamichezo mbalimbali wameweka kambi ambao wanamichezo wengine waliweka kambi katika nchi za Uturuki, China na New Zealand

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE