TWIGA AFA BAADA YA KUJIGONGA DARAJANI

Shirika la kutetea haki za wanyama la Afrika Kusini limeanza uchunguzi kuhusiana na kifo cha twiga baada ya kuumia wakati akisafirishwa kwenye gari. Watu walioshuhudia tukio hilo wanasema twiga mmoja kati ya wawili waliokuwa kwenye lori, aligonga kichwa chake katika barabara moja mjini Johannesburg. Gari hilo baadaye liliharibika na kulazimika kusubiri kwa saakadhaa kabla ya kutengenezwa.
Wanyama wote wawili walipelekwa kwa daktari wa wanyama, lakini shirika la kutetea haki za wanyama la NSPCA limesema twiga mmoja alikufa. Tukio hilo limeleta mjadala mkubwa kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter. Meneja wa NSCPA Rick Allen amethibitisha kuwa twiga huyo alipata majeraha ya kichwani lakini amesema uchunguzi ni muhimu ufanyike kutafuta sababu hasa ya kifo hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI