Hapa baadhi ya vigogo hao wakiwa ndani ya gari la polisi.
Maofisa wanne wa Chuo Kikuu cha
Kimataifa cha Matibabu na Teknolojia (IMTU), wakiwa chini ya ulinzi wa
Polisi nje ya Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni Dar es Salaam leo, baada
ya kusomewa mashitaka ya kushindwa kuizika kwa heshima miili ya binadamu
na kuonesha cheti kinachodhibitisha uzikaji wa miili hiyo. Baada ya
kusomewa mashitaka yao waliachiwa kwa dhamana na kukamatwa tena.
Hapa wakisindikizwa na askari polisi kwenda kupanda gari kurudishwa mahabusu ya Kituo Kikuu cha Polisi cha Kati.
Mmoja wa watuhumiwa hao akimsaidia mwenzake kupanda katika gari la polisi.
Comments