Unapozungumzia historia ya ulinzi na usalama wa kimkakati nchini Tanzania, Macho ya watu wengi mara nyingi huelekea miji mikuu au maeneo ya pwani. Hata hivyo, Ukweli wa kihistoria unathibitisha kuwa Iringa ndicho kitovu cha kweli cha ujasusi wa kizalendo na mbinu Mbalimbali kivita nchini.
Misingi hii haikujengwa juzi bali iliasisiwa mwishoni mwa karne ya 19 na mmoja ya wapelelezi nguli zaidi kuwahi kutokea katika ardhi ya Afrika Chifu Mkwawa wa wahehe.
Chief Mkwawa hakuwa shujaa wa vita vya msituni tu pia alikuwa ni gwiji wa ujasusi (espionage master) ambaye mbinu zake ziliwanyima usingizi wakoloni wa Kijerumani na kuweka mfumo thabiti ambao siri zake bado zinaishi katika medani za usalama hadi leo.
Mwishoni mwa-miaka ya 1880's, Jeshi la Kijerumani (Schutztruppe) lilikuwa na sifa ya Askari wake kuwa na nidhamu ya hali ya juu, Silaha za kisasa na mbinu za kisasa za kivita. Lakini walipokanyaga nyanda za juu kusini Mwatanzania katika Mkoa wa Iringa, walikutana na ukuta wa kijasusi ulioratibiwa kikamilifu na Chifu Mkwawa.
Ujasusi wa Mkwawa uliongozwa na nguzo kuu tatu, Moja ni Mtandao wa Informers (Watoa Habari) Chief Mkwawa alitandaza mamia ya wapelelezi wa siri, wakiwemo wanawake, wafanyabiashara, na wakulima, kuanzia Kilosa, Morogoro hadi Pwani ya Afrika Mashariki. Hakuna msafara wa Kijerumani ulioweza kusogea kuelekea Iringa bila Mkwawa kujua idadi ya askari, aina ya silaha walizonazo na muda wa kuwasili.
Pili, Chief Mkwawa alijua namna ya kutumia safu za Milima, Mabonde na Misitu ya Iringa kama ngao na mitego kwa wavamizi. Alisoma ramani ya ardhi yake kiufasaha kuliko adui yeyote.
Mwisho, Chief Mkwawa alikuwa na uwezo mkubwa wa kutunga habari za uongo (Counter-Intelligence) ili kuwapoteza maboya Wajerumani akiwavuta waingie kwenye maeneo ambayo walikuwa hawana msaada wa kimkakati.
Mapigano ya Lugalo (1891): Kilele cha Ujasusi wa Mkwawa ulionekana katika mapigano ya Lugalo (1891), Kamanda wa Kijerumani, Emil von Zelewski, aliongoza kikosi chenye silaha nzito akiamini anenda kumvamia Chief Mkwawa kwa kushtukiza. kabla wao hawajafika Chief Mkwawa alishajua ujio wao mapema kupitia wapelelezi wake. Alitega wanajeshi wake kwenye Nyasi ndefu za Lugalo, Pembeni kidogo mwa-njia ambayo wajerumani walikuwa wanapita.
Emil von Zelewski alijikuta ameingia katikati ya mdomo wa mamba bila kujua. Ndani ya dakika chache tu kikosi kizima cha Wajerumani kiliteketezwa na Zelewski aliuawa pale pale. Hili lilikuwa pigo kubwa sana uwahi kupatwa kwa majeshi ya kikoloni mikononi Mwa-waafrika wakati huo Shukrani zikienda kwa Early Warning Intelligence wa Mkwawa.
Nadhani watu wengi mmewahi kusikia sehemu inayoitwa Kalenga ngome ya siri ya Mawasiliano, Hata baada ya Wajerumani kurudi Iringa mwaka 1894 na kushambulia ngome ya Chief Mkwawa huko Kalenga, Lakini ujasusi wa Iringa haukufa Ngome ya Kalenga ilijengwa kwa mitindo madhubuti wa kiulinzi ambazo zilijumuisha mifumo ya dharura ya mawasiliano na njia za siri za kutokea chini ya ardhi (Maandaki).
Wajerumani walishangaa kuwa, pamoja na kuangusha ngome hiyo kwa mizinga mizito, lakini Chief Mkwawa alitoweka kirahisi na kuendesha vita vya msituni kwa miaka mingine minne. Katika miaka hiyo yote Wajerumani walishindwa kumkamata kwa sababu wahehe walikuwa na kiapo cha utii na usiri mkubwa ambayo ni nguzo kuu ya Ushirikiano wa kijasusi kati ya raia na jeshi (Civil-Military Intelligence).
Licha ya yote hao ni Makosa makibwa kufikiri kuwa ujasusi wa Wahehe uliishia baada ya kifo cha Mkwawa mwaka 1898. Iringa imebaki kuwa chimbuko na nembo ya usalama wa Tanzania kwa sababu kadhaa za kimkakati:
Mosi, Mbinu za Chief Mkwawa za kutumia rasilimali watu na jiografia kujilinda zimekuwa chemchemi ya mafunzo ya mbinu za medani na ulinzi wa taifa letu.
Pili, Utamaduni wa watu wa wanao fanya kazi ya Usalama wa taifa, Nidhamu, Utii na uwezo wa kutunza siri ni sifa ya sifa au miiko ya kazi hizo za kiintelijensia.
Leo hii Tanzania inasifika kwa kuwa na mifumo imara ya usalama na ujasusi inayolinda amani ya nchi yetu. Hata hivyo, Mti huu wenye matawi mapana una mizizi mirefu iliyozama ndani ya udongo wa Iringa chini ya Chief Mkwawa.

Comments