ADEN RAGE APATA AJALI DODOMA

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Simba, Mbunge wa Tabora Mjini, Aden Rage (CCM) akiwa amelazwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma baada kupata ajali leo katika eneo la Chigongwe, Manispaa ya Dodoma. Rage ambaye ameteguka mkono alikuwa natokea Tabora kwenda Dodoma kuhudhuria Bunge Maalum la Katiba.(PICHA NA MDAU WA KAMANDA WA MATUKIO)

Na Mdau Wetu
WABUNGE kutoka mkoa wa Tabora akiwemo Mbunge wa Viti Maalum Munde Tambwe (34) na Mbunge wa Tabora mjini Ismail Rage (60) wote wa CCM wamelazwa katika hospitali ya Rufaa  ya  Dodoma baada ya kupata ajali leo wakiwa wanatokea Tabora kuelekea Bungeni mjini Dodoma.

Ajali  hiyo imetokea katika eneo la Chigongwe katika Manispaa ya  Dodoma.

Akizungumza na waandishi wa habari Mganga Mkuu wa hospitali hiyo Ezekiel Mpuya alisema  wabunge hao  wamepokelewa pamoja na abiria wengine waliokuwa wamewabeba kwenye gari yao ambao ni Mwanahamisi Ramadhani (14) na John hoya (32). majira ya saa sita mchana.

Alisema  baada ya vipimo imeonesha  Munde amevunjika bega la kushoto na amepata majeraha kichwani huku Rage akiwa ameteguka   bega la kushoto.

Dk.Mpuya alisema majeruhi wengine wawili majibu ya vipimo bado yanasubiriwa.

"Majeruhi  wote  hali zao zao siyo mbaya na wanaendelea na matibabu,na kwamba baada ya muda wa siku chache watarejea katika afya zao za kawaida.

Akisimulia namna ajali ilivyokea Rage alisema,dereva wa hari yake alitaka kulipita gari la lililokuwa mbele yao na kusababisha ajali hiyo.

"Mbele yetu kulikuwa na gari ambalo lilikuwa linatembea nje ya barabara,sasa dereva wa gari yangu alipotaka kulipita lile gari ghafla waliona imeingia barabarani na wakati huo mbelw kulikuwa na gari lingine linakuja na hatimaye dereva wangu akaelekea kulia zaidi na kuacha njia,

"Dereva amefanya jitihada kubwa sana na tumashukuru Mungu ,maana ukiliona gari lilivyo ,huwezi kuamini kama  tumetoka katika hali tulizonazo." alisema Rage

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI