ESHA BUHETI WA BONGO MOVIE HALI YAKE NI TETE HOSPITALI

Mwigizaji, Esha Salim Buheti akiwa hoi kitandani.

MUIGIZAJI aliyelamba tuzo ya Muigizaji Bora wa Kike katika Tamasha la Zanzibar Festival Film ‘ZIFF’ mwaka huu, Esha Salim Buheti hali yake siyo nzuri na anahitaji maombi ili apone kutokana na kusumbuliwa na tatizo la uvimbe kwenye kizazi.Akizungumza na Ijumaa lililokwenda kumjulia hali katika Hospitali ya TMJ iliyopo Mikocheni jijini Dar, Esha alisema, alifikishwa hospitalini hapo juzi Jumatano akiwa na hali mbaya kufuatia ‘kuendesha’ ile mbaya. “Nilifikishwa hapa nikiwa na hali mbaya, nilikuwa ‘naendesha’ sana hadi kufikia hatua ya kuishiwa nguvu, ilibidi wanichukue vipimo ili kujua tatizo.

Akihudumiwa Hospitalini.
 “Baadaye wakaniambia nina uvimbe kwenye kizazi na UTI, yaani dah! Naomba Mungu anisaidie na naomba mashabiki wangu pia waniombee nipone,” alisema 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI