KIBOKO CHA MAN U, SWANSEA CITY WASAJILI BEKI LA ARGENTINA KOMBE LA DUNIA

KLABU ya Swansea City imekamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 8 wa Federico Fernandez kutoka Napoli.
Beki huyo wa kati alikwenda kufanyiwa vipimo vya afya wiki hii Wales na kusaini Mkataba wa miaka minne, akiweka rekodi ya kuwa mchezaji ghali zaidi wa nafasi za ulinzi kusajiliwa na klabu za Wales.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 25, ambaye aliichezea Argentina katika Kombe la Dunia, ataziba pengo la beki wa kati Chico Flores aliyeondoka, kwa kucheza na Ashley Williams.
Uhakika: Federico Fernandez akiwa ameshika jezi ya Swansea City baada ya kukamilisha uhamisho wa Pauni Milioni 8 kutoka Napoli

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI