Hebu Tulia na Ujionee Jinsi Maelefu ya Watu Walivyojitokeza Kwenye Tamasha la #Tuo8January Mjini Morogoro
Msanii
wa muziki wa kizazi kipya aitwaye Linah akiimba wimbo wake wa
OleThemba,mbele ya mashabiki wake (hawap pichani),waliojitokeza kwa
wingi kwenye tamasha la Tuo8January,lililofanyika kwenye viwanja vya
sabasaba jana jioni mjini Morogoro.
Mmoja
wa wasanii mahiri wa Hip hop,ambaye amekuwa akifanya vyema katika anga
ya muziki wa kizazi kipya, aitwaye Stamina akitumbuiza mbele ya umati wa
wakazi wa mji wa Morogoro katika tamasha la Tuo8January,lenye lengo la
kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki mchakato wa uchaguzi wa
viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta
mabadiliko ya kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.
Msanii
mwingine wa hip hop katika anga ya Bongofleva,ambaye amekuwa akifanya
vyema kwenye muziki huo,Niki wa Pili akitumbuiza katika jukwaa la wazi
la Tuo8Januari lililofanyika mjini Morogoro hapo jana.
Pichani
kati ni msanii Shilole akiwa sambambana madansa wake wakilishambulia
jukwaa kwa pamoja mbele ya umati wa wakazi wa mji wa
morogoro,waliojitokeza kwenye tamasha la Tuo8Januari,lililofanyika hapo
jana katika viwanja vya sabasaba mkoani humo.
Pichani
kulia ni Msanii Mwasiti akiimba wimbo wake wa serebuka akiungwa mkono
na shabiki wake kwa kunogesha zaidi jukwaa,huku shangwe za mayowe na
vifijo zikiwa zimetawala kutoka kwa mashabiki waliofika katika tamasha
la Tuo8January hapo jana.
Mkali
mwingine wa kughani mitindo huru, Godzilla akipanda katika jukwaa la
tamasha la Tuo8January,tayari kwa kuwaburudisha wakazi wa mji wa
Morogoro waliojitokeza kwa wingi katika tamasha hilo.
Baadhi
ya mashabiki wa muziki wa kizazi kipya wakifuatilia yaliyokuwa yakijiri
katika jukwaa la tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana katika
viwanja vya Sabasaba,mjini Morogoro.
Baadhi
ya wakazi wa mji wa Morogoro wakishangilia yaliyokuwa yakijiri kwenye
tamasha la Tuo8January,lililofanyika jana kwenye viwanja vya sabasaba
mjini humo,tamasha hilo la wazi ambalo limewashirikisha wasanii
mbalimbali,ni kampeni maalum ya kuwahamasisha vijana kushiriki katika
chaguzi mbalimbali kwa njia ya matamasha.
Kampeni
hiyo ilizinduliwa jijini Dar Desemba 10 mwaka huu
na kufanyika tamasha la kwanza mkoani Njombe na sasa Mkoani
Morogoro.Baadhi ya Wasanii mbalimbali wenye ushawishi mkubwa kwa vijana
wameonesha kuiunga mkono kampeni hiyo, akiwemo Babu Tale, Mwana FA, Nick
wa Pili, Lamar, P-Funk, Mwasiti, Barnabas, Ditto, G-nako, Fid Q,
Shilole, Yamoto Band, Stamina na wengineo.
Ilikuwa ni shangwe tu kutoka kwa mashabiki wa muziki wa kizazi kipya kupitia tamasha la Tuo8January
watazajamaji
wakifuatilia kwa umakini yaliyokuwa yakijiri katika jukwaa la
Tuo8January hapo jana katika uwanja wa sabasaba mjini Morogoro.
Sehemu
ya umati wa watu waliojitokeza kwenye tamasha hilo la la
Tuo8January,lenye lengo la kuwahamasisha vijana kujitokeza kushiriki
mchakato wa uchaguzi wa
viongozi mbalimbali wanaowataka na wanaowaamini wana uwezo wa kuleta
mabadiliko ya
kinidhamu kwenye masuala ya msingi ya Taifa letu.
Comments