Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepanga mikakati madhubuti ya kuhakikisha kwamba mkesha kuelekea Mwaka Mpya 2015
Kamanda wa Jeshi la Polisi Kanda Maalum Dar es Salaam, Suleiman Kova
--
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA
WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI
JESHI LA POLISI
Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam limepanga mikakati
madhubuti ya kuhakikisha kwamba mkesha kuelekea Mwaka Mpya 2015 unakuwa salama,
sherehe za mwaka mpya, kuandamana, baadhi ya watu wachache hasa vijana hupenda
kuchoma matairi barabarani, kulipua fataki na vurugu za kila aina kwa lengo la
kuonyesha furaha yao ya kuingia mwaka 2015.
Hali kama hiyo haitavumiliwa na Jeshi la Polisi kwa sababu badala
ya sherehe hugeuka vitisho, vurugu, na kisha kuwatia hofu wananchi wasiokuwa na
hatia. Katika harakati hizo Jeshi limeweka mpango kazi utakaowashirikisha
askari wa vikosi vyote pamoja na wadau mbalimbali watakaojihusisha na ulinzi
siku hiyo. Watakaojihusisha na ulinzi ni pamoja na kikosi cha Zimamoto, kampuni
binafsi za Ulinzi, na katika Jeshi la Polisi kutakuwa na kikosi cha FFU na
kikosi cha Mbwa na Farasi.
Kampuni binafsi za Ulinzi zitashiriki kikamilifu katika ulinzi huo
ambapo watafanya doria za miguu kwa pamoja, doria za magari, pamoja na askari
wa pikipiki. Baadhi ya watu hupenda kusherehekea mwaka mpya katika nyumba za
ibada ambapo Jeshi la Polisi litatoa ulinzi. Kutakuwa na ulinzi katika fukwe za
bahari pamoja na sehemu zote ambazo zinzkuwa na mikusanyiko ya watu wengi kama
vile katika Hotel kubwa kubwa na sehemu za wazi. Uwanja wa Taifa utalindwa
kutokana na mikusanyiko mkubwa wa watu utakaokuwepo siku ya mkesha pamoja na
viwanja vingine vyote vyenye mikusanyiko mingine kama hiyo.
Magari ya Zimamoto yatafanya doria yakisindikizwa na Jeshi la
Polisi ili kuhakikisha kwamba yeyote atakayejaribu kuchoma moto matairi au gari
atakamatwa na moto unazimwa.
Kutakuwa na ulinzi wa kutosha ufukweni mwa bahari ambapo Boti za
Polisi zitafanya doria ili kuwabaini wahalifu wa aina yoyote kutoka Baharini au
nje watakaojaribu kuingia na kufanya uhalifu jijini.
Helkopta ya Polisi itaanza doria kuanzia saa kumi na mbili jioni
ili kukagua maandalizi yoyote ya uchomaji moto au uhalifu mwingine wa aina
yoyote. Wananchi wanashauriwa kuwa makini na familia zao na hasa watoto wadogo
wasiruhusiwe kuingia barabarani wakati wa sherehe hizi kwani ni hatari kwa
maisha yao.
Madereva wajiepushe na ulevi ambao wanaweza kusababisha ajali
zisizo za lazima pindi wanapoendesha vyombo vya moto katika kipindi hicho.
Maafisa, Wakaguzi na Askari watakuwa “standby” kwa shughuli za ziada. Aidha,
kutakuwa na mwonekano wa askari wengi wa kila aina kabla na wakati wa sherehe
hizo ili kuhakikisha kwamba kuna amani na utulivu wakati wote wa kuingia mwaka
2015.
Wananchi wanaaswa kujihadhari na kufanya vitendo visivyo vya
kawaida kama vile kufyatua risasi za moto, kuendesha magari kwa mwendo kasi sana,
kupiga honi hovyo, au magari kuwa na milio ya kutisha yenye kero na badala yake
wafuate taratibu pamoja na kutii sheria bila shuruti.
Kinyume cha maagazo tajwa hapo, mtu yeyote atakayekaidi na kufanya
makosa ya jinai atachukuliwa hatua za haraka na hatimaye kufikishwa katika
vyombo vya sheria kwa mashtaka dhidi yake.
Ni muhimu pia wadau mbalimbali pamoja na wananchi kwa jumla kutoa
taarifa wakati ambapo kuna ishara ya uvunjifu wa amani au wakiwaona watu
wanaowatilia mashaka watoe taarifa kwa namba zifuatazo:
1. ZCO
- Constantine Masawe – SACP:0713-510 856 / 0658-111 100
2. RPC
ILALA – Mary Nzuki – SACP: 0715-009 980 / 0754-339 558
3. RPC
TEMEKE – Kihenya Kihenya – SACP: 0715-009 979 / 0754-397 454
4. RPC
K’NDON– Camillius Wambura – ACP: 0715-009 976 / 0684-111 111
S. H. KOVA,
KAMISHNA WA POLISI KANDA MAALUM,
DAR ES SALAAM.
Comments