Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ akiwa na mshindi wa shindano la Big Brothers Idris.
MWAKA 2014 unafikia tamati leo. Kwa Watanzania, kuna matukio
mbalimbali yaliyojitokeza ambayo yameacha kumbukumbu kubwa kwao. Hata
hivyo, yafuatayo ndiyo mambo yaliyotia fora zaidi. Viungo vingi vya binadamu vikiwa vimetupwa katika machimbo ya kokoto yaliyopo Bunju, Dar.
VIUNGO VYA BINADAMU VYASHTUA
Jumatatu ya Julai 21, 2014, nchi ilipatwa na mshtuko mkubwa baada ya
kusambaa kwa habari kuwa viungo vingi vya binadamu vilikutwa vikiwa
vimetupwa katika machimbo ya kokoto yaliyopo Bunju, Kinondoni jijini Dar
es Salaam.
Watu wengi waliamini viungo hivyo vimetokana na mauaji ya halaiki,
hasa baada ya kukutwa kwa mabaki ya mikono, miguu, mafuvu, viganja na
vingine vingi. Lakini baadaye ikaja kuthibitika kuwa viungo hivyo
vilitupwa kimakosa na Chuo Kikuu cha Kimataifa cha Tiba na Teknolojia
(IMTU), ambacho pia kinaendesha hospitali.
Viungo hivyo mbalimbali vya binadamu vilikuwa vikitumiwa kimasomo na
madaktari wanafunzi, ambavyo vilipaswa kuteketezwa baada ya matumizi.
Kitendo hicho kilisababisha serikali kukisimamisha kwa muda chuo hicho
kutokana na uzembe huo. Viungo hivyo vya binadamu, hupatikana katika
maiti mbalimbali zinazokosa ndugu wa kuwazika na hutolewa na hospitali
ya Taifa Muhimbili.
Baada ya Rais Jakaya Kikwete kuridhia zoezi la uandikwaji wa Katiba
Mpya, Tume ya kukusanya maoni chini ya uenyekiti wa Jaji Joseph Warioba
ilifanya kazi yake vizuri na mwaka huu katiba hiyo ilipelekwa Bungeni
ambako Bunge Maalum la Katiba lilikutana ili kupitia vifungu vyake kabla
ya kuipeleka kwa wananchi kwa ajili ya kuipigia kura ya kuikubali au
kuikataa.
Kulitokea malumbano makali kati ya wajumbe wa Bunge hilo juu ya
vipengele kadhaa, hasa muundo wa serikali ya Jamhuri ya Muungano.
Wajumbe waliotokana na Chama Cha Mapinduzi, walipendezwa na muundo wa
serikali mbili kama ilivyo hivi sasa, wakati wapinzani walitaka serikali
tatu.
Misimamo hiyo ilileta utengano mkali kiasi kwamba wajumbe wa upinzani
wakiongozwa na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba kuamua
kususia vikao hivyo, wakipinga kile walichokiita uchakachuaji wa rasimu
ya katiba ya Jaji Warioba. Ususiaji huo ulisababisha kuanzishwa kwa
kundi lililoitwa Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA).
Jaji
Warioba Kuanzishwa kwa umoja huo uliovihusisha vyama vya Chadema, CUF,
NCCR-Mageuzi na NLD, kulisababisha kundi hilo kukubaliana kusimamisha
mgombea mmoja katika chaguzi zijazo, wakianzia na uchaguzi wa serikali
za mitaa uliofanyika katikati ya mwezi huu.
JAJI WARIOBA APIGWA
Baada ya wajumbe wa Bunge Maalum la Katiba kumaliza kazi yake na
kuikabidhi katiba pendekezwa kwa Rais Jakaya Kikwete tayari kwa ajili ya
kuipeleka kwa wananchi ili kupigiwa kura ya maoni, kulikuwa na
mkanganyiko miongoni mwa watu juu ya kilichomo ndani ya katiba hiyo,
baadhi wakipinga kuondolewa kwa vifungu vingi vilivyokuwa na masilahi
kwa nchi.
Miongoni mwa wanaoongoza harakati za kupinga kuondolewa kwa baadhi ya
vifungu vilivyowasilishwa na Tume hiyo, ni Taasisi ya Mwalimu Julius
Nyerere ambayo mara kadhaa imeandaa mijadala ya wazi, lakini wakimtumia
Jaji Warioba kama msemaji wake mkuu.
Kitendo hicho kimesababisha Warioba kuonekana kama yupo katika
mgogoro na chama chake na siku aliyofanyiwa fujo na kupigwa katika
ukumbi wa mikutano wa Ubungo Plaza, wanaodaiwa kuwa makada wa CCM
wanatajwa kuhusika.
Aliyekuwa
mshindi wa miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu kabla ya kuvuliwa taji.
Kitendo hicho pia kilikosolewa na wachambuzi wa habari za kisiasa
wakidai ulikuwa ni udhalilishwaji wa mtu aliyewahi kuwa Makamu wa Rais
na Waziri Mkuu wa Tanzania na hivyo kuhoji ulinzi wake.MISS
TANZANIA YAFUNGIWA MIAKA 2
Shindano la Miss Tanzania limejijengea heshima kwa muda mrefu tokea
lilipoanza tena mwaka 1994. Ingawa kumekuwa na malalamiko ya chinichini
juu ya kuwepo kwa hila, safari hii lilijikuta likipata aibu kubwa, baada
ya mshindi wake wa mwakahuu, Sitti Mtemvu kudaiwa kudanganya umri hivyo
kuibua sauti zilizotaka kunyang’anywa kwa taji hilo.
Baada ya skendo hiyo kuchachamaa, Baraza la Sanaa la Taifa
liliendelea na uchunguzi wake dhidi ya malalamiko mengi yaliyowahi
kuripotiwa na katika tukio ambalo halikutarajiwa, shindano hilo
limesimamishwa kwa miaka miwili kutofanyika na sababu nyingine
iliyosababisha hatua hiyo, ni kugundulika kuwepo kwa rushwa ya ngono
katika hatua mbalimbali za shindano hilo linaloanzia vitongojini.
Aliyekuwa msanii mkongwe katika uchekeshaji maehemu Said Ng’amba ‘Mzee Small’. VIFO VYA WASANII WA MUVI NA MUZIKI
NI mwaka mwingine ambao wasanii wengi, wakiwemo wacheza filamu na
wanamuziki walifariki dunia. Mei 27 mwaka huu, msanii wa Bongo Muvi,
Rachel Haule alifariki katika hospitali ya Taifa ya Muhimbili. Alikwenda
hospitalini kwa ajili ya kujifungua, lakini baada ya kitendo hicho hali
yake ilibadilika ghafla ambapo alihamishiwa ICU na hali yake ilizidi
kuwa mbaya kabla ya kupoteza maisha.
Recho alifariki wiki moja baada ya muigizaji mwingine maarufu, Adam
Kuambiana kufariki ghafla. Baada ya hapo, msururu wa wasanii ulifuata
akiwemo prodyuza George Tyson, msanii mkongwe katika uchekeshaji Said
Ng’amba ‘Mzee Small’, mwanamuziki wa Twanga Pepeta, Khamis Kayumbu
‘Amigolas’, Side Mnyamwezi, Yesaya Ambilikile ‘YP’ , Maalim Gurumo,
Amina Ngaluma, Aisha Madinda na Shem Kalenga.
6. TEGETA ESCROW NA BILIONI 306
DAVID Kafulila, mbunge wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi) alianza kama
utani, akiwatuhumu vigogo wa serikali kuhusika na wizi wa shilingi
bilioni 306, mali ya umma katika akaunti ya Tegeta Escrow. Mwanasheria
Mkuu wa serikali wakati huo, Jaji Fredrick Werema akamdhihaki kwa
kumuita Tumbili kabla ya kumtishia kumkata kichwa. Dhihaka zikaendelea
kwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Eliakim Maswi, kuziita
nyaraka alizokuwa nazo Kafulila kuwa ni makaratasi ya kufungia vitumbua.
Mbunge
wa Kigoma Kusini (NCCR-Mageuzi), David Kafulila. Kadiri muda ulivyokuwa
unakwenda, ikaja kuthibitika kuwa ni kweli kulikuwa na uchotwaji wa
fedha hizo isivyo halali, kitu kilichosababisha nchi kuingia katika
kashfa nyingine ya mabilioni ya fedha, ukiacha EPA, Richmond, Rada na
Ndege ya Rais.
Mshindo wa skendo hiyo umeondoka na vigogo watatu, waliotanguliwa na
Jaji Fredrick Werema aliyejiuzulu, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo
ya Makazi, Profesa Anna Tibaijuka aliyeondolewa na Katibu Mkuu Maswi,
aliyesimamishwa ili kupisha uchunguzi dhidi yake.
HOMA YA DENGUE
Ni ugonjwa mpya ambao uliingia na kumshtua kila Mtanzania, kufuatia
kasi yake ya kuua na utata wa tiba yake. Uliwafanya watu kuogopa na
kuitaka serikali kuhakikisha tiba yake inapatikana mara moja ili kuondoa
hofu miongoni mwa wananchi.
8. UCHAGUZI SERIKALI ZA MITAA
INGAWA umekuwa ukifanyika kila baada ya miaka mitano, lakini uchaguzi
wa serikali za mitaa mwaka huu ulipata hamasa kubwa na kufuatiliwa kwa
karibu na watu wengi. Ingawa kama ilivyotegemewa, Chama Cha Mapinduzi
kuibuka na ushindi, lakini hata hivyo, matokeo yake yalionyesha dalili
za kuimarika kwa vyama vya upinzani baada ya kushinda viti takribani
3000 vya uenyekiti wa serikali za mitaa.
‘Diamond
platnumz’. Uchaguzi huo ambao ulisimamiwa na Tawala za Mikoa (TAMISEMI)
iliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu, ulikuwa na dosari kadhaa
zilizomlazimisha Waziri wake, Hawa Ghasia, kuwasimamisha kazi
Wakurugenzi, kuwafukuza na wengine kupewa onyo, kufuatia uzembe wao
katika kusimamia zoezi hilo muhimu nchini.
DIAMOND, IDRIS WANG’ARA
Msanii wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Diamond’ mwaka 2014 aliwaongoza
wenzake kuing’arisha Tanzania kimataifa baada ya kufanikiwa kutwaa tuzo
tano barani Afrika. Hizo ni pamoja na tatu kutoka kituo cha televisheni
cha Channel O, jijini Johannesburg na The Future Awards Africa
iliyofanyika Lagos, Nigeria.
Comments