SHEIKH SHARIF ATABIRI MGOMBEA URAIS 2015


Sheikh Shariff Matongo  akizungumza leo na waandishi wa habari ofisini kwake  jijini Dar es Salaam(hawapo pichani)kuhusu  ndoto yake ambayo ameoteshwa kuelekea mwaka 2015.
----
NA CHALILA KIBUDA,GLOBU YA JAMII,DAR.
Sheikh Sharif Matongo amesema ameoteshwa ndoto ya mwaka 2015 na kupata ushauri kwa mashekh mbalimbali duniani ambavyo vitatokea nchini na viongozi wasipuuze ndoto hiyo. Sharif aliyasema hayo leo ofisini kwake alipokutana na waandishi wa habari ,alisema ameoteshwa mambo saba likiwemo la kupata Rais ajaye ambaye kiongozi ambaye muda mwingi ameishi nje ya nchi kwa kufanya kazi.

Alisema katika ndoto nyingine kifo cha kiongozi mkubwa  ambaye ameshika nyadhifa mbalimbali na  na mwenye kambi katika Chama cha Mapinduzi (CCM). Sheikh  alisema ndoto nyingine  kutokea kwa mvua nyingi ambapo watu wanaoishi mabondeni ,kutokea kwa vifo vya watoto vingi ,wafanyabiashara kupata mafanikio  makubwa kwa mwaka utaoanza kesho.

Vijana wengi watashinda katika uchaguzi ujao na wazee wataangushwa sana ihivyo wanatakiwa kujitokeza,katiba inayopendekezwa  itapita lakini kutakuwa na vurugu ambazo zitaibuliwa na vijana.

‘’Ndoto yangu  niliopoteshwa sikukaanayo peke yangu niliweza kupata ushauri kutoka kwa watu mbalimbali akiwemo Mufti wa wa Abuu Dhabi,Mufti wa Nigeria  na wengine wote wakaniambia suala hilo nisikaaye nalo nishirikishe na watanzania wenzangu’’alisema Sheikh Shariff Matongo.

Sheikh Shariff alisema katika usafiri wa bahari utakuwa mbaya kutokana na bahari kuchafuka na chombo kimoja kitazama kutokana na kuchafuka huko.

Alisema ndoto hizo ni lazima kuweza kuzingatia kutokana na kupata ushauri wa watu wengi wenye kuaminika katika jamii katika mataifa mbalimbali ulimwenguni.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE

MONGELLA AKABIDHIWA ‘MIKOBA’ RASMI YA NAIBU KATIBU MKUU CCM BARA*

NCHIMBI AFUNGUA KONGAMANO LA MAADHIMISHO YA KUMBUKIZI YA MWALIMU NYERERE

MAKALLA ASHANGILIWA BUNGENI