MKUU WA WILAYA YA KINONDONI AZINDUA MAONYESHO YA TANO YA TANZANIA HOME EXPO

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akikata Utepe kuashiria Kuzindua Maonyesho ya Homes Expo ambayo yanafanyika kwa mara ya tano Katiaka Ukumbi wa Mlimani city Jijini Dar es salaam Sambamba akiwa na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup Ndugu Imani Kajula ambao ndio waandaji wa Moanyesho hayo yanayofanyika kwa siku tatu
Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Kutoka kwenye moja ya Banda washiki wa Maonyesho ya Home Expo  

 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akisikiliza kwa Makini maelezo Kutoka kwenye Mabanda ya Washiki Kwenye Maonyesho ya Homes Expo Akiwa Ameambatana na Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya EAGgroup Ndugu Imani Kajula Pamoja na Mkuu wa Masoko wa EAG group  Ndugu Richard Ryaganda ambao ndio waandaji wa Moanyesho hayo yanayofanyika kwa siku tatu
 Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda akipatiwa Maelezo Kuhusu Mradi mkubwa wa Ujenzi unaondelea katika Jiji la Dar es salaam Ujulikanao kwa Jina la Dege Eco Village.Katika Mradi huo Kijiji kinajengwa eneo la Kigamboni Jijini Dr es salaam ambao unahusha Ujenzi wa Nyumba za Makazi Ofisi sambamba na Huduma zote za Kijamii ikiwepo Shule,Hospitali na Nyinginezo Nyingi.

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akipatiwa maelezo Kutoka kwa Bi Linda ambaye ni Msimamizi wa Masoko kutoka Avic International  Real Estate Ambao nao wameibua Mradi mkubwa wa Ujenzi wa Makazi. 

 


Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Paul Makonda Akitoa wito kwa wakazi wa dar es salaam na Watanzania Kutembelea Maonyesho hayo Kupata Elimu aidi kwajili ya Maisha yetu ya kila siku kuhusu Makazi Bora .Mh Makonda akielezea zaidi amesema ni vema sasa watanzania kujikita kwenye maswala ya msingi na Yenye manufaa kwa taifa na kuangalia Fursa Mbalimbali zilizopo na kuzitumia ipasavyo na kuacha kuhangaika Na Mambo yasiyo na Msingi katika Maisha yetu ya Kila siku. 

Maonysho ya kila mwaka ya Homes Expo ambayo yanafanyika kwa mara ya tano, yameendelea leo katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam, yakiwa yameandaliwa na kampuni ya Eag- group.
Nchi zinazoshiriki maonyesho hayo mbali na wenyeji Tanzania ni pamoja na China, Uturuki, Ujerumani na Kenya.
Maonesho hayo yalianza juzi na yanatarjiwa kumalizika  Leo Mei 31 mwaka huu, huku Afisa Mtendaji Mkuu wa Eag-Group ambao ni waandaaji, Imani Kajula anawaomba wananchi kufika eneo hilo kujionea bidhaa na huduma mbalimbali zilizopo kwenye maonesho hayo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DK NCHIMBI ATINGA MKOANI KATAVI

BASHASHA LATAWALA NCHIMBI ALIPOLAKIWA NA CHONGOLO SONGWE