Katibu Mkuu Mstaafu Ofisi ya Rais –
Utumishi Bw. George D. Yambesi (aliyesimama) akizungumza katika hafla
ya kuagwa iliyofanyika viwanja vya Leaders Club jana jioni.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb)(kulia) akimkaribisha Katibu Mkuu
Mstaafu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. George D. Yambesi katika hafla ya
kumuaga iliyofanyika viwanja vya Leaders Club jana jioni.
Baadhi ya watumishi wa Taasisi
zilizo chini ya Ofisi ya Rais-Utumishi wakiwa katika hafla ya kumuaga
aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi
iliyofanyika Leaders Club jana jioni.
Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-
Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) akizungumza wakati wa hafla ya kumuaga
aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D. Yambesi (wa
pili kutoka kushoto) iliyofanyika Leaders Club jana jioni. Wengine ni
Mhe. Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais- Utumishi Bi.Celina O. Kombani (Mb)
(wa pili kutoka kulia) na Mama Yambesi (kushoto).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (kushoto) akizungumza wakati wa hafla ya
kumuaga aliyekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais-Utumishi Bw. George D.
Yambesi (hayupo pichani) iliyofanyika Leaders Club jana jioni. Kushoto
kwake ni Katibu wa Sekretarieti ya Ajira katika Utumishi wa Umma Bw.
Xavier Daudi.
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (Mb) (wa pili kutoka kulia) akionyesha
Tuzo ya Ununuzi Bora wa Umma ya Ofisi ya Rais – Utumishi iliyotolewa na
Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi ya Umma (PPRA) hivi karibuni baada ya
kushinda.Wanaoshuhudia ni Kaimu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw.
HAB Mkwizu (kulia) ,Katibu Mkuu Mstaafu Bw. George D. Yambesi (wa pili
kutoka kushoto) na Mama Yambesi (kushoto).
Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais –
Utumishi Mhe. Celina O. Kombani (wa pili kutoka kulia) akipokea kombe la
mshindi wa kwanza wa mpira wa pete la mashindano ya Mei Mosi 2015
kutoka kwa Kapteni wa Timu ya Netiboli ya utumishi Bi. Elizabeth Fusi
katika viwanja vya Leaders Club jana jioni. Wanaoshuhudia ni Kaimu
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais – Utumishi Bw. HAB Mkwizu (kulia) ,Katibu Mkuu
Mstaafu Bw. George D. Yambesi (wa pili kutoka kushoto) na Mama Yambesi
(kushoto
Comments