Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na Wananchi
na wanachama wa CCM Jimbo la Mkoani Mkoa wa kusini Pemba, katika uwanja
wa mpira wa Makombeni, mkutano huo wa hadhara wa kampeni za CCM
ulifanyika leo ikiwa ni mfulilizo wa mikutano inayoendelea
Maelfu
ya Wanachama cha Mapinduzi CCM na Wananchi waliofurika katika uwanja wa
mpira wa kijiji cha Makombeni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini
Pemba,wakinyoosha mikono yao juu kuunga mkono sera za CCM zilizotolewa
katika mkutano wa Hadhara wa kuwanadi wagombea wa nafasi mbali mbali za
Uongozi katika Chama cha Mapinduzi,wakiwemo Rais wa Zanzibar,Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,Wabunge ,Wawakilishi na Madiwani
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein akiwatambulisha wagombea
Udiwani wa CCM kwa Wananchi na wanachama wa CCM Jimbo la Mkoani Mkoa wa
kusini Pemba, katika uwanja wa mpira wa Makombeni, wakati wa mkutano
wa hadhara wa kampeni za CCM ulifanyika leo ikiwa ni mfulilizo wa
mikutano inayoendelea
Wananchi na WanaCCM pamoja na
Wapenzi wa Chama cha Mapinduzi wakisikiliza Sera za CCM zilizotolewa na
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi pia Makamo
Mwenyekiti wa CCM Zanzibar Dk.Ali Mohamed Shein wakati wa mkutano wa
Hadhara wa kampeni za Uchaguzi Mkuu uliofanyika leo uwanja wa Mpira
Makombeni Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba,
[Picha na Ikulu.]
Comments