VIMINI VYA MAOFISA WA SINGAPORE VYAZUA BALAA BUNGENI DODOMA


Na Richard mwaikenda, Dodoma.

VIMINI walivyo vaa baadhi ya maofisa wa kike wa Indonesia (pichani),  vimezua songombingo bungeni Dodoma jana.

Maofisa hao walikuwa miongoni mwa watu walioambatana na Waziri wa Viwanda na Biashara na Maendeleo ya Taifa wa Indonesia, Koh Poh Koon, ambaye alitambulishwa bungeni kuwa mgeni wa Waziri wa Viwanda na Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage.

Songombingo hilo lilizuka baada ya Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Godless Lema alipoomba muongozo kwa Naibu Spika na aliporuhusiwa alisema kuna baadhi ya wageni waliofika bungeni jana wamekiuka taraibu za Bunge kwa kuvaa nguo fupi.

Alisema imekuwaje wameruhisiwa kuingia bungeni wangali wameva vimini, wakati wabunge na wageni wengine sheria nataraibu za bunge zinawazuia kuingia wakiwa wamevaa nguo fupi.

Lema, alienda mbali, kwa kusema au ofisi ya Bunge inaogopa kuwaondoa bungeni kwa vile ni wazungu (weupe)? Alihoji huku akishangiliwa na baadhi ya wabunge.

Naibu Spika, Tulia Ackson, aliutolea majibu muongozo huo, kuwa sheria na kanuni za bunge hazisemi kuwa watu wanaingia bungeni wasivae nguo fupi yanii vimini bali inasema wavae nguo za heshima.

Baada ya Ackson kusema hivyo, likazuuka zogo huku baadhi ya wabunge wa upinzani wakizomea na CCM wakishangilia majibu hayo.

Wakati zogo hilo likiendelea, wageni hao waliokuwa wamevaa vimini walionekana kuendelea na mambo yao kwani walikuwa hawajui kuwa wanasemwa wao kutokana na lugha ya kiswahili iliyokuwa inatumika.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MATOKEO YA KIDATO CHA PILI, DARASA LA SABA YATANGAZWA ZANZIBAR

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

ZAIDI YA WANANCHI 500 KUSHIRIKI MAFUNZO YA MKIKITA YA KILIMO CHA PAPAI SALAMA

MKIKITA YATOA OFA KWA KILA HEKA YA PAPAI SH. MIL. 2 KUTANDAZA MIUNDOMBINU YA UMWAGILIAJI

WATEJA WA NSSF DAR WATIMULIWA KWA MTUTU WA BUNDUKI

DIAMOND AITWA NA NYOTA YAJAA GOMS

KAMISHNA MARIJANI AZINDUA CHAMA CHA WAFUGAJI MBWA TANZANIA (TCA)

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA