4x4

Taifa Stars yashindwa kuvunja rekodi yao mbaya dhidi ya Nigeria, yakubali kipigo mara ya tano


Jioni ya September 3 2016 timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars ndio ilihitimisha safari yake ya kuwania kucheza michuano ya mataifa ya Afrika 2017 maarufu kama AFCON,Taifa Stars iliyokuwa Kundi G lenye timu za MisriNigeria na Chad ambao walijitoa, imecheza mchezo wake wa kukamilisha ratiba dhidi ya Nigeria Super Eagles.
Taifa Stars ambayo ilicheza mchezo huo wa Kundi G kukamilisha ratiba sawa naNigeria, imekubali kipigo cha goli 1-0, goli  ambalo lilifungwa dakika ya 77 na nyota waNigeria anayeichezea Man City ya England Kelechi Iheanacho, hiyo ni baada ya kuishambulia Taifa Stars kwa muda mrefu.
Post a Comment