YULE MWANARIADHA WA BONGO ALIYEUMIA MWISHONI HUYU HAPA...Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) limesema kuwa sababu kubwa ya mwanariadha wa Tanzania, Emmanuel Giniki  kushindwa katika mashindano ya riadha ya mabingwa wa dunia mita 5,000 kulitokana na kuumia katika mzunguko wa mwisho.

Giniki aliongoza kwa mizunguko minne katika mbio hizo zilizofanyika juzi Jumatano jijini London, Uingereza, lakini alimaliza katika nafasi ya 13 akitumia muda wa dakika 13:32:31 nyuma ya mshindi wa kwanza, Muethiopia Yomif Kejelcha aliyetumia 13: 21: 50 huku bingwa wa zamani wa mbio hizo aliyeshika nafasi ya pili Muingereza, Mohamed Farah ‘Mo Farah’ akitumia muda wa dakika 13:30.07.

Akizungumza kutoka Uingereza, katibu wa shirikisho hilo, Wilhem Gidabudai alisema:  “Giniki amejitahidi ila tatizo hakuwa na uzoefu, alikanyagwa na spikes lep ya pili kuelekea mwisho, amepata majeraha, alipelekwa hospitali baada ya mbio lakini yupo salama.

“Kuhusu Gabriel Gerald Geay alikuwa na maumivu ambayo yalianza kupona na akawa anafanya mazoezi kwa umakini sana, ila siku mbili kabla  maumivu yalimzidia sana kutokana na  baridi, makocha na madaktari wa hapa kwenye ‘Sports Village’ wakaamua asikimbie maana uwanja ulikuwa unateleza sababu ya mvua,” alisema Gidabudai.
0

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

HIVI NDIVYO BIASHARA YA NGONO NAMNA INAVYOTIKISA MOROGORO: SEHEMU YA PILI.

LICHA YA UZURI WAKE MWANADADA ELIZABETH MICHAEL a.k.a LULU SI MALI KITU MBELE YA RAY, AMKWEPA KUOGOPA AIBU.

IJUE HISTORIA YA UHASIMU WA KOREA KASKAZINI NA MAREKANI

WAPENZI WANASANA WAKIFANYA MAPENZI GESTI

MATOKEO YA DARASA LA SABA YATANGAZWA

PICHA:NYOKA AINA YA CHATU AUWAWA KANISANI BAADA YA KUKUTWA NYUMBANI KWA MFANYABIASHARA MAARUFU JIJINI ARUSHA AKISADIKIWA KWA IMANI ZA KISHIRIKINA

WENGI WAJITOKEZA KUMUAGA MPENDWA WAO MWANAHABARI JOYCE MMASI